BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TASWIRA YA PICHA NANE ZA MANISPAA YA MOROGORO.

BW Hemed akiwa na mkewe Bi Habiba Yahaya mara baada ya kufunga ndoa iliyofanyika nyumbani kwa bibi harusi Bong'ola kisha kufuatiwa na sherehe kabambe ya kukata na mundu nyumbani kwa Bw harusi White House Kihonda Manispaa ya Morogoro, Bw Harusi ni mtumishi wa wizara ya mambo ya ndani wakati Bi harusi ni mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Morogoro.
 Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini kwa tikiti ya CCM, Abdullaziz Abood mbele akiwa katika mitambo ya kuchuja maji yanayotoka katika bwawa la Mindu kabla ya kwenda kwa watumia katika kituo cha kuchuja, kutibu na kuua wadudu cha Mafiga wakati wa ziara ya kutembelea miundombinu ya mamlaka ya majisafi na majitaka (Moruwasa) kufuatia hivi karibu mabomba ya wateja wa mamlaka hiyo kutoa maji yenye rangi ya kijana na matope ikiambana na harufu mkoani Morogoro
Kazi ni kazi ilimradi kinaingia kipato cha halali, msukuma mkokoteni Manispaa ya Morogoro akiwa na lundo la chupa tupu za maji ya kunywa akisafirisha kutoka sehemu moja kwenda nyingine akipita eneo la Msamvu Komoa kwa ajili ya kupeleka katika kituo ili kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam.
 Mfanyabiashara wa kuuza mboga mboga akiwa amepakia mboga hizo katika baiskeli mara baada ya kuzinunua katika soko la Mawenzi kisha kuzisafirisha hadi katika genge lake kwa ajili ya kuwauzia wateja wake kwa baei ya rejareja mkoani Morogoro.
 Gari ndogo likiwa limeharibika vibaya sehemu ya mbele baada ya kupata ajali eneo la Nanenane Mapumbani kwa kugongana na lori hata hivyo chanzo cha ajali hiyo haikuweza kufahamika mara moja mkoani Morogoro.
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiwa amemuweka chini ya ulinzi dereva wa bodaboda Kasheto Amos baada ya kutuhumiwa kumgonga mwendesha baiskeli katika makutano ya barabara ya Old Dar es Salaam na Nunge Hamza Ntigwa (80) kushoto muda mfupi kabla ya kupelekwa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro.
 Mwanafunzi Aisha Saidi (6) kushoto akijifunza namna ya kuandika namba hesabu huku mwenzake, Loveness Abubakari (3) kulia akiwangalia wakati wa somo la hesabu kwa wanafunzi wa shule ya awali kitengo cha viziwi shule ya msingi Kilakala Manispaa ya Morogoro.
Mkazi wa mji wa Ifakara wilaya ya Kilombero Michael Liganga akiwa amebeba kuni baada ya kuvuka nazo katika kivuko cha Mv 2 Kilombero wakati akirudi shamba lililopo katika wilaya ya Ulanga kufuatia kumaliza shughulizi za siku za kilimo mkoani Morogoro juzi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: