Mlinzi wa Yanga, SHEDRACK NSAJIGWA (katikati) akiwaongoza wenzake kufanya mazoezi mepesi kwa ajili ya maandalizi katika mchezo wao dhidi ya Polisi Moro SC katika uwanja wa jamhuri kesho.
Saimon Msuva akiajiandaa kupiga krosi wakati wa mazoezi hayo jioni hii uwaja wa Jamhuri Morogoro. Wachezaji wa Yanga pamoja na kocha wao wakiomba dua mara baada ya kumalizika kwa mazoezi katika uwanja wa jamhuri jioni hii.
Wachezaji wa Yanga wakimzonga mchezaji mwenzao Shedrack Nsajigwa kwa utani wakati wa mazoezi hao.
Kocha mkuu wa klabu ya Polisi Moro SC Mohamed Adolf Richard akiwaeleza jambo wachezaji wake kwa ajili ya mchezo wao na Yanga kesho.
Salum Machaku akifanya mazoezi na kocha wake Mohamed Richard juzi jioni katika uwanja wa jamhuri Morogoro
Nahodha wa Polisi Moro SC Mokili Lambo akiongoza mazoezi mepesi kwa wachezaji wenzake kwa ajili ya kujiweka fiti dhidi ya Yanga kesho.
Mshambuliaji wa Polisi Moro SC Nicolaus Kabipe kulia akipiga mahesabu ya kumpokonya mpira mchezaji mwenzake Bantu Adimini wakati wa mazoezi hao.
0 comments:
Post a Comment