JIJI la Dar es Salaam limegubikwa na simanzi nzito kufuatia
kuanguka kwa jengo la ghorofa 16 lililopo Mtaa wa Indira Ghandi leo
asubuhi.
Ajali hii mbaya imesababisha vifo vya watu 2 na
kuacha idadi isiyofahamika, wakiwemo wajenzi na wapita njia, wakiwa
wamekwama ndani ya kifusi.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam Suleiman Kova amewaambia waandishi wetu kuwa waokoaji
wamefanikiwa kunusuru watu 15 wakiwa hai.
Taarifa zilizotufikia zinaongeza kuwa magari
matatu yameteketea baada ya kuangukiwa na masalia ya jengo hilo,
lililokuwa likijengwa na kampuni ya Lucky Construction Limited.
Katika harakati za kuhamasisha shughuli za uokoaji, Rais Jakaya Kikwete, Mwananchi imeelezwa, amewasili katika eneo la tukio.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa shughuli za uokoaji
zinakwamishwa na vifaa duni, pamoja na jitihada za ziada kutoka kwa
maofisa wa jiji wakishirikiana na Jeshi la Kujenga Taifa na kampuni
binafsi ya ulinzi ya Ultimate Security.
Tutawaletea taarifa zaidi kadiri zinavyotufikia
0 comments:
Post a Comment