Kwa ufupi
Fundi ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa katika
Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada ya
jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
http://www.mwananchi.co.tz
Rais Kikwete na Mkewe, Mama Salma Kikwete wakimpa pole Yusuph Abdallah
katika Hospitali ya Muhimbili walipotembelea majeruhi wa ajali ya
kuporomoka jengo la ghorofa 16. Picha na Muhidin Michuzi.
DAR ES SALAAM.
FUNDI ujenzi, Yusuph Abdallah ambaye amelazwa
katika Taasisi ya Mifupa (Moi), ameeleza jinsi alivyonusurika kifo baada
ya jengo la ghorofa 16 kuporomoka Ijumaa iliyopita.
Yusuph aliliambia Mwananchi akiwa wodini kwamba
kilichomponya ni neema za Mungu kwani kabla jengo hilo kuporomoka yeye
alikuwa ghorofa ya 15 kwenye jengo hilo katika Mtaa wa Indira Gandhi
akiendelea na ujenzi.
Alieleza kuwa hakuwa anafahamu kinachoendelea,
bali aliona ghafla jengo linaaanza kuporomoka, na baada ya hapo
hakufahamu zaidi kilichotokea hadi alipojikuta yuko hospitalini.
“Kweli jengo lilipoanza kuporomoka sikutambua nini
kinachoendelea kwani nilipoteza fahamu na kujikuta nipo hapa
Muhimbili,” anasimulia Abdallah.
Alisema anahisi alipoanguka alifunikwa na kifusi kilichomponda na kuvunja miguu yote.
Fundi huyo ambaye amefungwa plasta gumu (P.O.P) miguu yote, alisema hakuweza kuona watu waliomwokoa.
Mwingine aokolewa na mkewe.
Mkazi wa Ubungo, Ally Mlela ambaye ni fundi
madirisha anasimulia jinsi mke wake alivyomwokoa katika ajali hiyo baada
ya kumtaka asiende kufanya kazi siku hiyo.
Akisimulia jinsi ilivyokuwa Mlela anasema siku ya
tukio aliwasiliana na rafiki yake ambaye amepoteza maisha katika ajali
hiyo na kumtaka aende akaonane na mkandarasi wa jengo hilo, ili ampe
kazi ya kuweka madirisha.
“Majira ya asubuhi kati ya saa mbili na saa tatu
hivi nilipokea simu kutoka kwa rafiki yangu jina maarufu anajulikana
kama Tafu, ambapo alinitaka niende nikaonane na mkandarasi wa jengo hilo
ili anipe kazi ya kuweka madirisha,” anasema Mlela.
Anasema wakati akijiandaa kutoka mke wake
alimwambia siku hiyo apumzike asiende kufanya kazi naye akakubali,
lakini haikupita muda mrefu mke wake alimfuata na kumuuliza amesikia
taarifa kwamba kuna jengo limedondoka ?.
“Niliamua kwenda katika eneo la tukio na ndipo
alipogundua kwamba eneo hilo ndiyo alipotakiwa kwenda kufanya kazi.
Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea nilijaribu tena kumpigia simu rafiki yangu.
Nikiwa bado kwenye eneo la tukio ghafla nikaona mguu ukitolewa kwenye mchanga na nilitambua ulikuwa mguu wa rafiki yangu baada ya kuona kiatu chake.”
Wakati juhudi za uokoaji zikiendelea nilijaribu tena kumpigia simu rafiki yangu.
Nikiwa bado kwenye eneo la tukio ghafla nikaona mguu ukitolewa kwenye mchanga na nilitambua ulikuwa mguu wa rafiki yangu baada ya kuona kiatu chake.”
0 comments:
Post a Comment