BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AZAM SASA YAIPUMULIA YANGA SC, YAITANDIKA AFRIKA LYON 3-1 CHAMAZI.

Wachezaji wa Azam wakimpongeza mfungaji wa mabao yao mawili, Kipre Tchetche (katikati) jioni ya leo Chamazi 

Na Mahmoud Zubeiry
AZAM FC imepunguza ‘gepu’ la pointi inazozidiwa na vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC hadi kubaki tatu, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 jioni ya leo dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.


Mabao ya Azam katika mchezo wa leo, yalitiwa kimiani na Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya tisa na Kipre Herman Tchetche dakika za 28 na 61, wakati la Lyon lilifungwa na Adam Kingwande dakika ya 36.

Pamoja na kufungwa, Lyon ilionyesha upinzani kwa Azam FC na kufanya mchezo uwe mtamu.

Kipigo hicho kinazidi kuiweka Lyon katika hatari ya kushuka daraja, ikibaki na pointi zake 19, baada ya kucheza mechi 23 na sasa ni miujiza tu itakayoifanya timu hiyo iendelee kucheza Ligi Kuu msimu ujao.

Azam itashuka tena dimbani Jumapili, kumenyana na mabingwa watetezi Simba SC katika mfululizo wa ligi hiyo.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Azam kilikuwa; Aishi Manula, Himid Mao, Wazir Salum, Luckson Kakolaki, Joackins Atudo, Jabir Azizi, Kipre Tchetche, Abubakar Salum, Abdi Kassim/Seif Abdallah, Ibrahim Mwaipopo/Humphrey Mieno na Khamisi Mcha/Brian Umony.

African Lyon; Noel Lucas, Ibrahim Isaac, Sunday Bakari, Yussuf Mlipili, Obinna Salamusasa, Juma Seif/Hamadi Manzi, Jackob Massawe, Mohamed Samatta, Adam Kingwande, Freddy Lewis/Alphonce Lucas na Ndela Kashakala/Bright Ike.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: