BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHEZEA JK !!!, WALIOMWOMBEA ITIKAFU RAIS KIKWETE ILI AFE WATUBU.


KATIKA hotuba yake ya mwisho wa mwezi Machi, Rais Jakaya Kikwete pamoja na mambo mengine alizungumzia kwa uchungu tatizo la udini linaloonekana kulitafuna taifa kwa kasi, kiasi cha watu kuanza kutoana roho.
Kilichonishangaza zaidi ni pale aliposema kuwa kuna misikiti mitatu ya jijini Dar es Salaam, ambayo iliamua kumwombea itikafu ili afe.

Swali la kujiuliza hapa ni je, Mungu wanayemwomba atimize matakwa yao ya kumtakia rais mabaya ni huyo huyo tunayemfahamu na kumwabudu sote au ni Mungu mwingine anayefurahia fulani kupatwa na mabaya?

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, misikiti hiyo ilimwombea itikafu afe kwa madai kwamba, amekuwa akishiriki kwenye shughuli za Wakristo zaidi kuliko zile za Waislamu.

Waumini hao wamesahau kuwa Rais Kikwete hakuchaguliwa kwa misingi ya kidini, bali utaifa.



Hawa walioamua kukaa na kuswali ili eti Rais afe, wanatakiwa kuomba msamaha kwa Mungu wao kwa sababu walichotenda ni dhambi iwapo Mungu wanayemwamini ni huyu tumjuaye, vinginevyo wana Mungu mwingine.

Ni kwa sababu Mungu tunayemwabudu Waislamu na Wakristo, hawezi kusikiliza sala za namna hiyo, vinginevyo matakwa yao yangekuwa yamesikilizwa.

Rais Kikwete katika hotuba yake hiyo, alifafanua kwamba amekuwa akishiriki katika shughuli zote za Waislamu na Wakristo bila ubaguzi.

Hata hivyo, aliweka wazi kuwa amekuwa akipata wasaa mzuri zaidi kushiriki mazishi ya Wakristo kwa sababu ya imani yao, mtu anapofariki inachukua muda kidogo kabla ya kumzika na hivyo yeye kupata muda wa kujiandaa tofauti na dini ya Kiislamu ambayo huzika mapema.

Alitoa mfano kuwa anapopata taarifa ya msiba wa Kiislamu akiwa nje ya nchi, inakuwa ngumu kuwahi msiba huo tofauti na ile ya Wakristo ambayo marehemu huwa bado hajazikwa.

Pamoja na hilo la rais kuombewa itikafu afe, ikiwa ni siku chache tu baada ya kutoa hotuba yake hiyo, tulishuhudia vurugu kubwa katika Mji wa Tunduma mkoani Mbeya, jambo ambalo lilisababisha shughuli za uchumi kusimama.

Vurugu hizo zilizuka baada ya baadhi ya wakazi wa mji huo, kuingia mitaani na kufanya vurugu kubwa za kufunga barabara, kuchoma magurudumu ya magari na kuharibu baadhi ya nyumba za ibada.

Chanzo cha vurugu hizo inadaiwa ni mgogoro baina ya Wakristo na Waislamu kuhusiana na nani anastahili kuchinja wanyama.

Tukio linalofanana na hili nalo liliwahi kutokea huko Buseresere mkoani Geita, ambapo Mchungaji Mathayo Kachila, aliuawa kutokana na mzozo kati ya Wakristo na Waislamu kuhusu kama nyama iliyochinjwa na Wakristo kanisani nayo iuzwe kwenye bucha iliyopo pale kijijini ambayo kwa mazoea huuzwa nyama iliyochinjwa na Waislamu.

Watu kadhaa walijeruhiwa na mchungaji huyo kupoteza maisha kutokana na mzozo huo.

Swali la kujiuliza ni je, hawa wanaohangaika na kuibua haya mambo hawana shughuli za kufanya? Kwa sababu mtu ambaye anaamka asubuhi kwenda kutafuta riziki najua hawezi kuwa na muda huo wa kuhangaikia mzozo huo hadi kujiingiza kwenye vurugu kama hizo. Hilo nalo litazamwe.

Nashauri wakati ufike sasa wa Serikali pamoja na viongozi wa dini, kukaa pamoja na kuzungumzia suala hili ili kufikia muafaka na busara itumike katika hili vinginevyo taifa litafika pabaya na itakuwa ni aibu kubwa kama watu wanaacha kufanya mambo ya msingi na kuhangaikia kuchinja wanyama.

Katika hili pia wanasiasa wanapaswa kuchunga kauli zao, na kuingiza itikadi za vyama vyao kwani nao wanatajwa kuchangia vurugu za sasa zinazotokana na chuki za kidini. http://www.mtanzania.co.tz
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: