Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na
wakuu wa Vikosi vya ulinzi alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM
Kisdiwandui Mjini Unguja kuhudhuria katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar
Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
Wananchi
na Waumini wa Dini ya Kiislamu wakisoma Hitma Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,katika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya
CCm Kisiwandui Mjini Zanzibar,ambapo kila ikifika siku kama hii wananchi kwa
ujumla wao hukusanyika kuomba dua kama hii.
Wake wa Viongozi Wakuu wakiwemo na viongozi wa taasisi za Kinamama wakinyanyua mikono juu kumuombea dua Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.katika kaburi lake huko CCM Kisiwandui mjini Zanzibar,baada ya kisomo cha Hitma leo Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume,(kulia) akiwa na Wake wa Viongozi mbali mbali katika Hitma ya Rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,huko Ukumbi wa CCK Kisiwandui Mjini Zanzibar Leo.
Akina
mama wa Kiislamu wa Mjini Magharibi Unguja wakijumuika na Viongozi
wengine katika kisomo cha HItmaya Kumuombea Dua Rais wa kwanza wa
Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume,leo katika ukumbi wa Ofisi ya
CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.




0 comments:
Post a Comment