BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUTANO WA DOHA NA MPANGO WA KULIJENGA UPYA JIMBO NCHINI QATAR .

Kambi ya Kalma ya wakimbizi wa ndani, Darfur 
WAWAKILISHI wa nchi wahisani na mashirika ya misaada wanakutana leo mjini Doha, Qatar ili kuunga mpango wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kulijenga upya jimbo la Darfur.

Kiongozi wa ujumbe wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Jorg kuhnel amesema mkutano huo ni fursa ya kipekee kwa Sudan ya kuweza kuibadilisha hatma ya jimbo hilo lililokumbwa na migogoro.

Mkutano huo wa siku mbili, unaohudhuriwa na wajumbe 400, unafanyika kwa mujibu wa mkataba wa amani wa Julai mwaka 2011, uliotiwa saini mjini Doha baina ya Sudan na mfungamano wa makundi ya waasi.

Mkutano huo unafanyika miaka kumi baada ya waasi katika jimbo hilo la magharibi mwa Sudan kuanzisha harakati za kukomesha walichoita udhibiti wa mamlaka na mali, wa viongozi wa kiarabu nchini Sudan.

Uhalifu wa Janjaweed :
Ili kuwakabili waasi ,wanamgambo wa Janjaweed waliokuwa wanaungwa mkono na serikali ya Sudan walitenda unyama dhidi ya raia,ulioishtua dunia na kuifanya Mahakama ya Kimataifa ya mjini The Hague itoe hati ya kisheria ya kuwezesha kumkamata Rais wa Sudan Omar al-Bashir kwa tuhuma za kutenda uhalifu wa kivita,uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji halaiki.
Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir.
 
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo Bwana Kuhnel ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, baada ya miaka kumi ya kutegemea misaada ya dharura,wakati sasa umefika wa kuanza kuzijenga upya jamii za Darfur na kuwawezesha watu wa jimbo hilo kujihudumia wenyewe.

Uingereza yaahidi Pauni milioni 11 kwa mwaka:
Katika hatua ya kwanza,Uingereza imetoa ahadi ya kuchangia Pauni Milioni 11 kila mwaka kwa ajili ya jimbo la Darfur kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na kwa ajili ya mafunzo yatakayowawezesha watu kupata ajira.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron.
 
Waziri wa Uingereza anaeshughulikia misaada ya maendeleo ya kimataifa Lynne Featherstone amesema haitoshi tu ,kutoa ruzuku zaidi. 

Waziri Featherstone ameeleza kuwa fedha hizo zitawasaidia masikini kupata nyenzo wanazohitaji ili kuweza kujisimamia wenyewe na hivyo kuzikabili vizuri zaidi hali za migogoro zinapozuka.

Maendeleo ya kilimo:
Mpango utakaofadhiliwa na wahisani na mashirika ya kimataifa ni pamoja na kuboresha kilimo, kuwawezesha watu kupata misaada ya fedha na kuchukua hatua ili kuwasaidia watu wa Darfur kujisimamia wenyewe chini ya uongozi wa mfumo wa serikali ya jimbo hilo ,unaofanyakazi kwa ufanisi zaidi. 

Mkakati wa maendeleo ya jimbo la Darfur,unasisitiza kwamba wakati wa kuchukua hatua ni sasa, kwani kuchelewa kutasababisha mchakato huo uwe mgumu.

Hata hivyo wakati mikasa mibaya ya umwagikaji wa damu imeshapita, waasi na wanajeshi wa serikali wanaendelea kupambana,sambamba na mapambano baina ya jamii za kiarabu.

Wakati mgumu lakini hapana kushika tama
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maendeleo,UNDP Bwana Kuhnel amekiri kwamba hizi ni nyakati ngumu duniani kukusanya fedha.Lakini amesema litakuwa kosa kubwa kutoitumia fursa iliyopo duniani.
Nembo ya UNDP Nembo ya UNDP.
 
Ameeleza kuwa, siyo lazima fedha zote zinazohitajika zipatikane mara moja. 

Ameeleza kwamba kinachohitajika ni kuanza juhudi na kupata kiasi cha fedha kitakachojenga imani ya mkakati unaokusudiwa kutekelezwa.

Usalama kwanza nyumbani:
Wakati huo huo wakimbizi wa ndani katika jimbo la Darfur,katika kambi kadhaa, walifanya maandamano kabla ya mkutano wa Doha kuanza kusisitiza ulazima wa kulipa kipaumbele suala la usalama.

Watu hao wamesema kuwa hawatarejea kwenye vijiji vyao kabla ya amani kurejea.

Justice and Equality Movement:
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alisema mapema mwaka huu kwamba kukataa kwa makundi muhimu kuutia saini mkataba wa Doha kumepunguza hatua za utekelezaji wa mkataba huo.

Kundi moja lililojitenga na chama cha "Justice and Equality" hapo jana(Jumamosi) lilikuwa kundi la pili kujiunga na mkataba wa Doha. Lilitiliana saini mjini Doha "makubaliano ya mwisho" na serikali ya Sudan.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: