BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HOSNI MUBARAK AREJESHWA JELA BAADA YA KUTOKA HOSPITALINI MISRI

Kiongozi wa mashtaka aliamuru Mubarak kurejeshwa jela baada ya kuonekana mwenye nguvu na kiwapungia mkono wafuasi wake.
Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak.Hosni Mubarak
ALIYEKUWA rais wa Misri, Hosni Mubarak, amerejeshwa jela kutoka hospitalini mjini Cairo.

Shirika la habari la nchini humo MENA limesema kuwa bwana Mubarak alipelekwa hospitalini viungani mwa mji wa Cairo akiwa chini ya uilinzi mkali.

Kiongozi wa mashtaka nchini humo aliamuru Mubarak kurejeshwa jela baada ya kuonekana mwenye nguvu huku akiwapungia mkono wafuasi wake.

Kesi ya mauaji ya waandamanaji dhidi yake itaanzishwa upya mnamo Jumatatu.

Maperma wiki hii mahakama iliamuru Mubarak kutolewa jela baada ya ombi la wakili wake kuwa miaka miwili imepita kabla ya kesi dhidi ya Mubarak kutofanyiwa uamuzi wowote katika kipindi hicho.

Chini ya sheria za Misri mtu hawezi kuwa jela zaidi ya miaka mahakama ikiwa haijatoa uamuzi katika kesi inayomkabili.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: