Kwa ufupi
Maugo aliyewahi kupigwa na Cheka mara kadhaa
huku akitoa visingizio mbalimbali, alisema kuwa anataka Cheka ashinde
katika raundi ya nne ya pambano hilo dhidi ya Mashali.http://www.mwananchi.co.tz
DAR ES SALAAM.
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, bondia namba tatu hapa nchini, Mada ‘King’ Maugo amemuombea ‘hasimu’ wake Francis Cheka kutetea taji lake la IBF Afrika na kutaka ashinde kwa Knock Out (KO) dhidi ya Thomas Mashali kesho.
Maugo aliyewahi kupigwa na Cheka mara kadhaa huku akitoa visingizio mbalimbali, alisema kuwa anataka Cheka ashinde katika raundi ya nne ya pambano hilo dhidi ya Mashali.
Cheka atatetea taji hilo kesho dhidi ya Thomas Mashali katika pambano la raundi 12 la uzani wa Super Middle (kg 76) litakalopigwa kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mabondia hao leo watapima uzito na afya tayari kwa pambano hilo lililobeba hisia za mashabiki wengi wa mchezo huo hasa kutokana na Mashali kuamua kupandisha uzito ili azichape na Cheka anayeshikilia namba moja ya ubora katika ngumi hapa nchini.
“Nitakuwa upande wa Cheka Jumat
ano (kesho) nataka Mashali apigwe ikiwezekana raundi ya nne kwani yule bado ‘mtoto’ kwenye ngumi,” alisema Maugo katika mahojiano na Mwananchi.
Maugo ambaye ana rekodi ya kupigwa kwa TKO raundi ya saba wakati akigombea taji hilo na Cheka alibainisha kuwa licha ya kutomkubali Cheka, lakini kesho atakuwa upande wake kwenye pambano hilo na kumuombea ashinde.
Bingwa wa pambano hilo ataondoka na gari aina ya Noah yenye thamani ya Sh 12 Milioni.

0 comments:
Post a Comment