Mbunge wa jimbo la Bumbuli mkoa wa Tanga, January
Makamba kushoto akizungumza na baadhi ya wananchi wake katika jimboni hilo hivi
karibuni.
MBUNGE
wa Bumbuli kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), January Makamba, ameelezea
kusikitishwa kwake na masuala ya imani ya kishirikina kupiga hodi kwenye Jimbo
lake.
Akielezea
kwa kina kwenye akaunti yake ya facebook, Makamba alisema kuwa Ijumaa na
Jumamosi walikwenda Bumbuli watu wanaodai wana uwezo wa kutoa wachawi na kuamua
kuwachangisha watu fedha kwa ajili ya zoezi hilo na kudhalilisha wazee na kina
mama wengi na kusababisha wanyanyaswe na kufanyiwa fujo.
Alisema
kuwa baada ya kuona hivyo, aliamua kuzungumza na viongozi na Mkuu wa Wilaya
kwamba watu hao wafukuzwe mara moja na wakamatwe kwasababu zoezi hilo ni
kinyume cha Sheria za nchi.
"Vilevile,
katika zama hizi mambo ya uchawi na kutafuta
wachawi hayana nafasi kabisa. Ni mambo ambayo yametubakiza nyuma kimaendeleo
miaka nenda rudi.
"Baada ya witch-hunters
kufukuzwa kuna baadhi ya vijana walioratibu ujio wao walienda kituo cha polisi
Bumbuli na kujaribu kung'oa dirisha na kuvunja mlango. Kituo cha Polisi
hakijachomwa moto. Pia wakaenda kwenye Ofisi ya Afisa Tarafa na kujaribu
kuvunja Ofisi," alisema Makamba.
Aliendelea
kusema kuwa wote wamekatwa Jumapili na kupata message nyingi za wapiga kura
wakimpongeza kwa kuzuia upuuzi na wengine wakitaka waruhusiwe watoa uchawi.
"Kama
viongozi, tunayo kazi kubwa ya kuelimisha watu kuhusu hizi imani.
Changamoto
kwetu kule sio tu masuala ya barabara, maji, umeme, nk lakini pia haya masuala.
Bahati mbaya imani za kichawi zimeshamiri sana kwenye jamii nyingi za Kiafrika
na kazi ya kuziondoa ni kubwa sana.
"Mara nyingi zinatokana na maendeleo kuwa duni
lakini vilevile imani hizo ni chanzo cha maendeleo duni. Hadithi ya kuku na yai
kipi kilianza, bahati nzuri hali imetulia. Kilifanyika kikao cha Madiwani wote,
wenyeviti wote wa vijiji na Watendaji wa Kata na Maafisa Tarafa kuweka msimamo
wa pamoja kuhusu haya masuala ikiwemo elimu kwa umma," alisema.
0 comments:
Post a Comment