Kwa ufupi
“Mwaka juzi tulitaka fedha ziongezwe Wizara ya
Uchukuzi na Serikali ikasema imeongeza Sh94 bilioni na tukapiga makofi
sana hapa, lakini haikuongezwa hata senti moja.”
http://www.mwananchi.co.tzMbunge Bunge wa Ubungo, John Mnyika akizungumza wakati Bunge lilipokaa kama
kamati kwa ajili ya kupitisha mafungu ya fedha ya Bajeti ya Wizara ya
Maji kwa Mwaka wa Fedha 2013/14, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin
Mjwahuzi
DODOMA.
BAJETIi ya Wizara ya Maji jana ilipita kwa mbinde baada ya kukwama mara mbili bungeni.Imepita baada ya Serikali kuongeza Sh184.5 bilioni kama Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ilivyokuwa imependekeza na kuungwa mkono na wabunge wengi.
Awali, Bajeti hiyo ilikwama kupitishwa tena
katika kipindi cha jana asubuhi baada ya Spika wa Bunge, Anne Makinda
kukatiza mjadala wake kutokana na wabunge kuibana Seri
kali kwa kukiuka vipengele kadhaa wakati ilipowasilisha upya hoja hiyo.
kali kwa kukiuka vipengele kadhaa wakati ilipowasilisha upya hoja hiyo.
Mara ya kwanza Bajeti hiyo ilikwama wiki
iliyopita baada ya wabunge kushinikiza kuongezwa kwa fedha kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya kusambaza maji vijijini.
Jana asubuhi, Makinda alisitisha shughuli za
Bunge saa 5.45 asubuhi ikiwa mapema kabla ya muda wa kawaida wa
kumalizika kwa vipindi vya asubuhi ya Bunge ambao ni saa 7.00 mchana
baada ya wabunge kupinga utaratibu wa uwasilishaji upya wa Bajeti hiyo.
Licha ya Serikali kuongeza Sh184.5 bilioni, bado
baadhi ya wabunge wa Chadema waliomba Bajeti hiyo iahirishwe kujadiliwa
wakisema nyongeza hiyo haina ushahidi wa utekelezaji.
Baada ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa
kuwasilisha kauli ya Serikali kuhusu kuongeza fedha kwenye Bajeti ya
Wizara ya Maji na Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe kusoma
marekebisho ya bajeti yake na kujibu hoja mbalimbali za wabunge, Mbunge
wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe alihoji sababu za Serikali
kuwasilisha kauli ya kuongeza fedha bila kuwagawia wabunge nakala kama
kanuni zinavyotaka.
“Mwaka juzi tulitaka fedha ziongezwe Wizara ya
Uchukuzi na Serikali ikasema imeongeza Sh94 bilioni na tukapiga makofi
sana hapa, lakini haikuongezwa hata senti moja.”
Pia, Zitto alisema mwaka 2011 walikubaliana fedha
zinazotokana na ushuru wa mafuta ya taa kupelekwa Wakala wa Umeme
Vijijini (Rea), lakini hakuna kilichopelekwa mpaka sasa.
Kutokana hali hiyo, alitaka hoja hiyo kutolewa kwa maandishi na wabunge wapewe nakala zake ili waibane Serikali pale itakaposhindwa kutekeleza.
Kutokana hali hiyo, alitaka hoja hiyo kutolewa kwa maandishi na wabunge wapewe nakala zake ili waibane Serikali pale itakaposhindwa kutekeleza.
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu
Lissu ambaye alitinga bungeni baada ya kutumikia adhabu ya kusimamishwa
kwa siku tano, alisema kwa mujibu wa taratibu za Bunge, kauli za
Serikali lazima zisambazwe kwa wabunge tofauti na kauli ya Waziri wa
Fedha akisema hata Spika hakuwa na nakala yoyote huku akisema Waziri
alitoa kauli hiyo akiwa hana anachokisoma.
Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alitaka
hoja hiyo kuondolewa mezani kwa sababu Waziri wa Maji wakati akifanya
majumuisho ya hoja yake, hakutoa jedwali linaloonyesha matumizi ya fedha
hizo.
Akitoa mwongozo wake, Spika Makinda alisema
Waziri wa Fedha alitoa tamko la Serikali bila wabunge kuwa na nakala
kutokana na haraka iliyokuwapo... “Tuliona haiwezekani Waziri wa Maji
aseme peke yake juu ya ongezeko la fedha hizo, ndiyo maana Waziri wa
Fedha akaja kutoa tamko hapa.”
Hata hivyo, Makinda alikubaliana na hoja ya
Mnyika na kuahirisha Bunge huku akitaka jedwali linaloonyesha matumizi
ya fedha hizo liandaliwe.
0 comments:
Post a Comment