Kwa ufupi
“Hatukuzuia ziara yake hata kidogo, yeye aliomba
kufanya ziara ya kichama na wakati huo tulikuwa tunazuia mikutano ya
vyama vyote,” alisema Pinda.
http://www.mwananchi.co.tz
DODOMA. YAMETOLEWA malalamiko bungeni kuwa Serikali imemzuia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad kufanya ziara mkoani Mtwara.
Madai hayo yalitolewa na Mbunge wa Mkanyageni
(CUF), Mohamed Habib Mnyaa wakati akiuliza swali katika kipindi cha
Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu.
Mnyaa aliitaka Serikali itoe kauli yake kuhusu mawaziri ambao wamekuwa wakiruhusiwa kwenda mkoani humo bila kizuizi.
Mnyaa aliitaka Serikali itoe kauli yake kuhusu mawaziri ambao wamekuwa wakiruhusiwa kwenda mkoani humo bila kizuizi.
Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
alisema Serikali haikumzuia Maalim Seif, bali ilikuwa inatekeleza agizo
lake la kuzuia shughuli za kisiasa mkoani humo.
“Hatukuzuia ziara yake hata kidogo, yeye aliomba
kufanya ziara ya kichama na wakati huo tulikuwa tunazuia mikutano ya
vyama vyote,” alisema Pinda.
Alisema shughuli hizo zilizuiliwa ili kutoa nafasi
kwa Serikali kufuatilia hali iliyokuwapo mkoani humo na kuahidi kuwa
baadaye mambo yataendelea kama kawaida.
Katika swali la nyongeza, Mnyaa alitaka kujua ni
lini zuio hilo litamalizika ili vyama vya siasa viendelee na shughuli
zake kwa kuwa vimesajiliwa kisheria.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema haitachukua muda
mrefu, hali itatulia na vyama vya siasa kikiwamo CCM, CUF na vingine
vitaruhusiwa.
Hivi karibuni kulizuka vurugu mkoani Mtwara baada ya wananchi kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam, hali ambayo Serikali iliihusisha na uchochezi wa kisiasa.
Hivi karibuni kulizuka vurugu mkoani Mtwara baada ya wananchi kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam, hali ambayo Serikali iliihusisha na uchochezi wa kisiasa.
Vurugu hizo zilikwenda mbali zaidi kwa watu wa
Mtwara kufanya maandamano makubwa na siku nyingine kufanya vurugu
zilizoambatana na kuchomwa kwa ofisi za Serikali, Mahakama na nyumba za
baadhi ya wabunge na viongozi wa mkoani Mtwara.
0 comments:
Post a Comment