Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Katibu Mkuu wa taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Khamis Mataka alisema hatua hiyo ya kuwakutanisha viongozi hao, itasaidia kulinda amani ya nchi kwa njia ya mazungumzo.
Sheikh Mataka, alisema hatua hiyo ya Mufti ni muhimu ambayo alianza kuinyoosha kupitia mkutano wa mano na uvumilivu ulioandaliwa na taasisi hiyo Februari 20, mwaka huu.
“Taasisi ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu, tunawaomba viongozi wa dini ya Kikristo watoe ushirikiano katika kufanikisha dhamira njema ya Mufti na kwamba bila ushirikiano wao ni vigumu kuirejesha afya ya jamii inayozorota kila uchao katika hali njema,” alisema Sheikh Mataka.
Akizungumzia ziara ya Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ulimwengu wa Kiislamu (RABITA), Dk. Abdullah Al-Turki, alisema kuwa zimekuwa na mafanikio makubwa kwa nchi.
0 comments:
Post a Comment