Rais wa mpito atatawala kw akipindi kisichopungua miezi 18, wakati ambapo baraza hilo la mpito lenye wanachama 105 litachukua nafasi ya baraza la katiba.
Baraza hilo linajumuisha maafisa wa Seleka, wajumbe wa utawala uliondolewa na vile vile wawakilishi wa mashirika ya kiraia.
Majirani wa Jamhuri ya Afrika ya kati na washirika wa magharibi wameonya kuwa wasingetambua utawala wa Djotodia, lakini pia hawaonyeshi nia ya kuunga mkono kurejea kwa kiongozi aliepinduliwa, Francois Bozize.
Ni taarifa kidogo tu zinazofahamika kuhusu kiongozi huyo mpya wa taifa hilo lisilo na pwani, lililo na utajiri mkubwa sana wa madini, ambao hata hivyo haujaguswa, na linaendelea kuwa moja ya mataifa maskini zaidi duniani.
Baada ya miaka kadhaa kama mtumishi wa umma na mwandiplomasia, Djotodia aliepata mafunzo yake nchini Urusi, ambae alizwaliwa mwaka 1949, aligeukia uasi na kuanzisha vuguvugu la kijeshi mwaka 2005, m iaka miwili baada ya Bozize kuchukua madaraka kupitia mapinduzi.
Changamoto zinazomkabili
"Nafahamu umuhimu wa kazi mlioniamini kuifanya.
Nitafanya kila juhudi kuhakikisha ufanisi wa serikali ya mpito ambayo imeanza kazi yake hivi sasa," Djotodia alisema katika hotuba yake rasmi ya kwanza kama kiongozi siku ya Jumamosi.
Alisema changamoto ambazo atakabiliana nazo katika miezi michache ijayo ni pamoja na kujenga upya umoja wa kitaifa, kuhakikisha usalama nchini kote, kurejesha amani ya kijamii na kufufua uchumi.
Mashambuli za muungano wa Seleka yalioanza Disemba mwaka jana yalisababisha machafuko na uporaji ambavyo hadi sasa havijaweza kudhibitiwa.
Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambayo ina ukubwa sawa na Ufaransa, lakini yenye wakaazi milioni tano tu, imejaa silaha na utulivu unaonekana kuikwepa nchi hiyo, ambako serikali kuu imekuwa ikipambana mara kwa mara kuweka mamlaka yake nje ya mji mkuu.
Djotodia amesisitiza kuwa ataendelea kuwa muaminifu kwa kanuni za makubaliano ya amani ya Januari 2013, yaliyofikiwa kati ya muungano wa Seleka na utawala wa Bozize.
Awali kiongozi huyo alitangaza kuwa angetawala kwa amri kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi, lakini jumuiya ya kimataifa ilishinikiza kuwekwa taasisi za mpito na ratiba inayobana.
Kura ya Jumamosi inatazamiwa kuirudisha Jamhuri ya Afrika ya kati katika msitari, baada ya Umoja wa Afrika kuisimamisha uanachama na wafadhili kusitisha misaada kwake.
Jamhuri ya Afrika ya Kati inategemea zaidi msaada kutoka nje.
0 comments:
Post a Comment