BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA JIMBO LA MORO MJINI AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO VYA ZAIDI YA SH 10 MIL MOROGORO.

Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Mourice Massala kulia akimkabidhi seti ya jezi kiongozi wa timu ya soka ya Power Stone FC ya mail moja Mkundi, Frank Charles wakati wa hafla ya kutoa msaada wa seti za jezi ambapo zaidi ya sh10 mil zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa seti za jezi kwa timu mbalimbali katika Manispaa ya Morogoro.
Katibu wa mbunge wa jimbo la Morogoro mjini, Mourice Massala kulia akimkabidhi seti ya jezi kiongozi wa timu ya soka ya Kings Of Lova,
James Mkenda akikabidhiwa vifaa.

Sehemu ya viongozi wa timu hizo wakiwa na vifaa vya michezo baada ya kukabidhiwa. Picha JUMAMTANDA.BLOG

Na Juma Mtanda, Morogoro.
OFISI ya mbunge wa jimbo la Morogoro mjini imetumia kiasi cha sh10 Mil kwa ajili ya ununuzi wa seti za jezi za mchezo wa soka kwa ajili ya kuzipatia msaada timu za mchezo huo lango likiwa ni vijana kuendelea kuibuka na vipaji vya mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi katika hafla ya kutoa msaada wa seti za jesi za mchezo wa soka katika ofisi ya mbunge huyo mjini hapa Katibu wa mbunge Mourice Massala alisema kuwa mpaka sasa kuna zaidi ya sh10 Mil zimetumika katika ununuzi wa seti za jezi za mchezo wa soka kwa timu mbalimbali mkoani hapa.

Massala alisema kuwa utoaji wa seti za jesi kwa timu mbalimbali katika Manispaa ya Morogoro umezingatia zaidi kwa timu changa ambazo hazina uwezo wa kununua vifaa vya michezo.

Timu zilizokabidhiwa jezi hizo katikia hafla hiyo ni pamoja na Mindu SC,Lugala FC, Magadu SC, Urugwai FC, Nungutu FC, Chamwino SC, Mawenzi FC,Visole SC, BHT FC, na Kings Of Love.

“Mpaka sasa kuna zaidi ya seti za jezi 50 tumekabidhi kwa timu zikiwa na thamani ya zaidi ya sh10 Mil ambapo jezi hizo zina wastani wa sh 250,000 kwa seti moja ikiwemo na mipira miwili au mmoja kwa timu na lengo kuu ni kuwahamasisha vijana kupenda mchezo wa soka ikiwemo na kuibua na kuendeleza vipaji vya mchezo wa soka katika jimbo la Morogoro mjini
Alisema Massala.

Massala alisema kuwa baada ya kutoa seti hizo za jezi kwa timu za soka kumesaidia kupunguza vijana kujiingiza katika makundi ya uhalifu ambapo wengi wamekuwa wakijikita katika mchezo wa soka asubuhi na jioni.

Naye Kiongozi wa timu ya soka ya Kings of Love FC ya Areasix kata ya Kichangani James Mkenda alisema kuwa kupata msaada wa seti wa jezi hizo umesaidia kuokoa kiasi cha sh5,000 ambacho timu yake ilikuwa ikikodi jezi kwa ajili ya kuzitumia katika mchezo mmoja pindi wanaposhiriki ligi mbalimbali za mchezo wa soka.

Mkenda alisema kuwa kwa sasa baada ya kupata msaada huo wataelekeza nguvu katika mchezo wa soka ili kuweza kuendeleza na mpango wa timu hiyo ya kuibua na kuendeleza vipaji vya mchezo wa soka kwa wachezaji ili kuweza kupata nafasi ya kuingia katika timu kubwa ikiwemo Polisi Moro SC na Mtibwa Sugar zinazoshiriki ligi kuu ya vodacom na timu nyingine.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: