Korir alishinda mbio za Boston Marathon mwaka 2012.
MSHINDI wa mbio za mwaka 2012 za Boston Marathon,
Wesley Korir, aliyemaliza wa tano mwaka huu, ameambia BBC kuhusu hofu
yake pindi aliposikia milipuko miwili iliyotokea Boston Marekani.
Milipuko hiyo ilitokea karibu na msitari wa
mwisho wa kumalizia mbio hizo na kuwajeruhi takriban watu 140 takriban
saa mbili baada ya mshindi kumaliza mbio hizo.
''Ikiwa shambulio hilo lingetokea saa mbili kabla ya mbio kumalizika
labda ningekuwa miongoni mwa waliojeruhiwa,'' alisema bwana Korir.
Alikuwa akisherehekea ushindi wa mkenya Rita Jeptoo katika mbio za wanawake.
"furaha yetu ni kuwa tulikuwa tayari tumeondoka katika eneo hilo,'' Korir aliambia BBC.
Bi Jeptoo anatoka katika eneo bunge la
Cherangany, ambalo bwana Korir ni mbunge wake baada ya kushinda katika
uchaguzi uliofanyika mwezi jana.
Licha ya milipuko hiyo pamoja na jukumu lake la
kisiasa, Korir amesema kuwa ataendelea kushindana katika mbio za
marathon hata ikiwa Boston itaandaa mbio zengine mwaka ujao.
Korir alisema kuwa aliogopa sana aliposikia kuhusu habari ya milipuko.
Alisema kuwa punde tu baada ya kusikia habari
hiyo aliwapigia simu wakwe zake kuwajulia hali kwani walikuwa
wamemtembelea pamoja na kocha wake.
Balozi wa Kenya nchini Marekani amesema kuwa hana taarifa zozote kuhusu wakenya waliojeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.
Raia wawili wa Afrika Kusini walitibiwa baada ya kupata majeraha.
Lelisa Desisa, wa Ethiopia alishinda mbio za wanaume mbele ya mshindani wake Micah Kogo.
Mbio hizo mwaka huu zilikuwa na wanariadha 23,000 na zilitazamwa na mamia ya mashabiki.
0 comments:
Post a Comment