Taasisi
ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo imeanza mkutano
wake wa 27 wa mwaka kwa watafiti Wanasayansi jijini Arusha ambapo Makamu
wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein anataraji kuufungua rasmi jioni ya leo.
Pamoja na
Mkutano huo wa NIMR, pia mkutano wa pili wa Wanasansi kuhusiana na
Masuala ya Afya barani Afrika unafanyika sambamba na mkutano huo ambapo
watafiti mbalimbali duniani wanatoa mada juu ya tafiti mbalimbali za
magonjwa ya binadamu.
Mkutano
huo ambao umebeba kauli Mbiu ya Mabadiliko ya Mazingira katika Utafiti
wa Afya 'Changing landscape in Health Research' utafanyika kwa siku nne
katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha.
Pichani
ni Dk. Jeff Waage kutoka Uingereza akiwasilisha mada juu ya Kilimo na
Afya katika Mabadiliko ya Mazigira katika Utafiti wa Afya.
Washiriki |
Baadhi ya
washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia mada
mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha hii leo. Baadhi ya
Wabunge nao wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment