POLISI katika jimbo la Massachusetts wanaendelea na msako mkali wa
mmoja wa washukiwa wa mabomu ya Jumatatu katika mji wa Boston baada ya
kumuuwa mwingine katika majibizano ya risasi Alhamisi usiku.
Vyombo vya
habari Marekani vinaripoti kuwa washukiwa hao ni ndugu wenye asili ya
Chechnya.
Maafisa wanasema mshukiwa aliyekuwa amevaa kofia nyeupe kwenye milipuko
ya kwenye mashindano ya riadha, ajulikanaye kama mshukiwa namba mbili
hajulikani alipo na anaripotiwa kuwa hatari na mwenye silaha.
Polisi
wanawaasa wakazi wa Watertown kiasi cha kilometa 8 kutoka Boston,
wakae ndani na wasifungue milango yao kwa mtu yeyote isipokuwa Polisi.
Polisi wanakwenda nyumba hadi nyumba kumtafuta mshukiwa huyo.
Shirika la habari la NBC linaripoti kuwa washukiwa hao wawili ni ni
ndugu, mtu na kaka yake wenye asili ya Chechnya. Shirika la AP
linasema wanatoka kwenye jimbo moja karibu na Chechnya.
Vyombo vya habari vya Marekani vinasema ndugu hao walikuwa wakiishi
Marekani kihalali na mshukiwa ambaye anatafutwa sasa ni Dzhokar
Tsarnaev mwenye umri wa miaka 19.
Maafisa wanasema mshukiwa mmoja aliyepigwa picha na FBI akiwa na kofia
nyeusi alijeruhiwa vibaya na risasi Alhamisi usiku na kufariki baada ya
kupelekwa hospitali.
Mshukiwa alikuwa akirusha vifaa vya milipuko
wakati akijaribu kukimbia.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment