Mmoja
wa washukiwa wawili wa tukio la ulipuaji bomu katika mbio za Marathon
huko Boston, Marekani ameuawa kwa risasi huku polisi wakiendelea
kumsaka mwingine.
POLISI wa jimbo la Massachusetts wamewaonya wakazi wa Watertown, kujifungia
ndani mwao na wasimfungulie milango mtu huyo anayeaminika kuwa ni
gaidi.
Wamesema mtu huyo ni hatari na ni tishio kwa kila mtu
anayemsogelea.
Picha za washukiwa hao zimetolewa na FBI jana.
Tangazo
hilo limekuja masaa kadhaa baada ya jana usiku kwenye mitaa ya
Watertown kutokea tukio la kurushiana risasi ambapo polisi mmoja
aliuawa kwenye campus ya chuo cha teknolojia cha Massachusetts, MIT.
Kupitia akaunti yake ya Twitter (MASS STATE POLICE @MassStatePolice) polisi wa jimbo hilo iliandika:
“If
any concerns about someone at door, call 911 immediately.
Repeat–Do
not answer door, stay away from windows, keep doors locked.
Residents in and around Watertown should stay in their residences.
Do NOT answer door unless it is an identified police officer.
Police
will be going door by door, street by street, in and around Watertown.
Police will be clearly identified. It is a fluid situation.”
0 comments:
Post a Comment