Mmoja wa washukiwa wa mashambulizi ya Boston
POLISI nchini Marekani wanamsaka mshukiwa mkuu wa
mashambulizi yaliyotokea katika mbio za Boston Marathon katika mji mdogo
karibu na Boston.
Mshukiwa mmoja aliuawa baada ya polisi kumfukuza hali iliyosababisha ufyatulianaji wa risasi umbali wa kilomita kumi kutoka Boston.
Mshukiwa mwingine ambaye picha yake ilionyeshwa alikuwa amevalia kofia huku akikimbia kutoka eneo la Watertown.
Polisi walisema kuwa wanaume hao wawili walishukiwa kumuua polisi mmoja, katika chuo hicho cha Massachusetts Jumanne jioni. Thursday.
Baadaye waliiba gari mmiliki wake akiwemo ndani kwa kutumia nguvu lakini walimwachilia mmiliki bila kumjeruhi.
Shirika la FBI limetoa picha kadhaa za washukiwa hao.
Wawili hao waliwasrushia polisi mabomu na hata kwuafyatulia risasi kabla ya kusimamishwa katika eneo la Watertown.
Wakaazi wa mtaa huo wameshauriwa kusalia makwao.
0 comments:
Post a Comment