BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SPIKA MAKINDA AKIPIGILIA MSUMARI WA MWISHO ADHABU YA WABUNGE WA CHADEMA


Leo asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu Mh Spika ametoa uamuzi kuhusu muongozo ulioombwa na Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kuhusu uhalali wa kutolewa nje na kisha kufungiwa vikao vitano kwa wabunge sita (6) wa Chadema uliotolewa juzi na Naibu Spika. Mh Spika anasema kwa kuwa kwa sasa hakuna kanuni kuhusu jambo hilo.

Uamuzi wa Naibu spika utabaki halali na utaingizwa kwenye kumbukumbu za bunge kwa ajili ya kutumika huko mbele kwa ajili ya maamuzi pale itakapotokea tukio kama hilo.

 
Kwa uamuzi huo Wabunge hao watakosekana bunge bunge kwa siku tano ambazo ni Alhamisi (jana), Ijumaa (leo) pamoja na Jumatatu, Jumanne na Jumatano wiki ijayo.
 

Uamuzi wa Naibu Spika Mh. Job Ndugai, wa kumtoa nje Mh. Lissu, Mh. Sugu na wengineo, na kupewa adhabu ya kutoshiriki vikao vitano vya Bunge, Kutokana na Mh. Tindu Lisu Kuomba Muongozo/Taarifa mara kwa mara, Hivyo Kuingilia wengine katika kutoa hoja zao, na baadae kitendo cha wabunge hao kukaidi amri Halali ya Naibu Spika ya kutoka nje ya Bunge pamoja na kuwagomea Askari wabunge.

Kitendo ambacho kidogo kizue masumbwi live, Umebarikiwa na Mheshimiwa Spika kwa kufuata kanuni za Bunge, Hivyo Basi, Maamuzi ya Mh. Ndugai, yatakua Kanuni Rasmi kwa Tukio kama Hilo Na adhabu iliotolewa.
Photo
Taswira ya vurugu zilizotokea bungeni dodoma jana ambapo Mbunge wa mbeya Mh mbilinyi akiskiwa pamoja na wenje, lema na wengineo wakionekana kwa pamoja wakiwazuaia askari ili wasimtoe nje mh Tundu lissu aliyeamriwa na naibu spika atolewe nje ya ukumbi wa bunge

hapa waziri wa nchi na uratibu wa bunge Mh William Lukuvi akiwaeleza jambo wabunge wa chadema mara baada ya kikao cha bunge kuahirishwa baada ya kutokea vurugu bungeni
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: