Rais wa
Marekani Barack Obama ameikana ziara ya rapa nyota nchini humo Jay- Z na
mke wake Beyonce akisema kuwa hana habari na safari yao waliyoifanya
hivi karibuni kwenda nchini Cuba
Hivi karibuni Jay Z na Beyonce
walisafiri kwenda nchini Cuba kwa ajili ya kuadhimisha miaka mitano ya
ndoa yao jambo lilolosababisha maofisa wa Chama cha Republican kutaka
ufanyike uchunguzi ama amevunja vikwazo vya kusafiri
Akiwa nchini humo rapa huyo
alizindua kibao chake alichokipa jina la'Open Letter' ambacho mashahiri
yake yanaonekana kama Obama alikuwa amemzuia kufanya ziara hiyo,hata
hivyo taarifa iliyotolewa na Msemaji wa White House, Jay Carney ilieleza
kuwa utawala wa Serikali ya Rais Obama ulitoa baraka zote kuhusu safari
hiyo ya Jay Z kwenda Cuba na kwa sasa rais huyo ametoa kauli kama hiyo
0 comments:
Post a Comment