L Mwenyekiti wa Kata na wenzake 68 watimkia CCM
Wadai Chadema imekubuhu kwa utapeli.
Wadai Chadema imekubuhu kwa utapeli.
NA BASHIR NKOROMO, GAIRO
TSUNAMI ya ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM, mkoani Morogoro imeiacha CHADEMA taaban wilayani Gairo baada ya
Mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Mkalama wilayani hapa, Zefania Magiga
na wenzake 68 kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara jana,
Aprili 18, 2013.
Magiga na wenzake walikabidhi kadi
zao za Chadema kwa Kinana, na kupewa kadi za CCM, baada ya kutangaza
kukihama chama chao na kujiunga na CCM kwenye mkutano huo ambao
ulifurika mamia ya wananchi, kwenye Uwanja wa shule ya Msingi Gairo B,
katika wilaya mpya ya Gairo.
Mbali na kupokea wanachama hao
kutoka Chadema, kwenye mkutano huo, Kinana alipokea wanachama wapya 120,
waliojunga na CCM na kufanya jumla ya wanachama wapya waliojinga na CCM
kwenye mkutano huo kuwa 188.
“Ndugu wana Gairo wenzangu na Watanzania wote, mimi kwa nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Kata, nilikuwa naongoza wanachama wengi wa Chadema, na nilikuwa si mtu mdogo, lakini kwa muda ambao nimekuwa ndani ya chama hicho nimebaini kuwa viongozi wake wa kitaifa ni matapeli wa hali ya juu, ndiyo maana mimi na wenzangu tumeamua kuhamia CCM”, alisema Magiga.
Alisema, akiwa Chadema alikuwa
akishangaa kuona kwamba kila agizo alilokuwa akipokea kutoka viongozi
hao wa chama hicho lilikuwa na kumwagiza kushawishi wananchi shari na
kukataa kutii sheria za nchi, jambo ambalo alisema kwa muda mrefu
akikuwa hakubaliano nalo kwa kuwa ni tofauti na lengo lililokuwa
limemwingiza Chadema tangu kuanzishwa kwake miaka zaidi ya 15 iliyopita.
“Kwa kuwa sasa nnimeamua kurejea rasmi CCM, na hawa wenzangu (67) nimewaelimisha kwamba Chadema ni chama hatari nao wakanielewa sasa leo tunahamia wote CCM tunaomba mtupokee bila kinyongo, maana kufanya kosa si kosa kosa ni kulirudia”, alisema Magiga baada ya kukabidhiwa kadi yake ya CCM na Kinana.
Akizungumza kwenye mkutano huo,
Katibu Mkuu wa CCM, alisema, uoamuzi wa wananchi wanaojiunga na CCM sasa
na hata baadaye ni wa busara sana kwa sababu CCM ndicho chama ambacho
bado cha kuaminika kwa malengo na matarajio yote ya maendeleo, amani na
usalama wa Watanzania.
Kinana aliwataka wananchi wa Gairo
na Tanzania kwa jumla kuendelea kuiunga mkono CCM ili iendelee
kuwatumikia kwa kuwa bado ni chama imara kutokana na kuasisiwa katika
misingi ya uhakika.
Mapema kabla ya mkutano huo, Kinana
alifika katika kata mbalimbali wilayani Gairo na kufungua mashina ya
Wajasiriamali wakereketwa wa CCM, ambapo pamoja na kuyafungua
aliwahimiza kushina hayo kama kicocheo cha kufanya shughuli mbalimbali
za maendeleo kwa lengo la kukuza uchumi wao na wa taifa.
“Tunapofungua mashina haya
hatukusudii kuwa vijiwe vya kupigia soga tu, bali tunawataka wanachama
wetu wa CCM myatumie kukaa pamoja na kuunda vikundi vya ushirika na
kuanzisha shughuli za uzalishaji mali ambazo zinawatoa kwenye kulalamika
kwamba hakuna ajira kwa kuwa mtakuwa tayari mnazo shughuli za kufanya”,
alisema Kinana.
Kinana alifungua zaidi ya mashina
saba, abayo aliawaahidi wanachama wake kuwapa ushirikiano mkubwa katika
kuwasaidia kuinuka kiuchumi ambapo baadhi aliahidi kuwapa fedha au
vitendea kazi kwa ajili ya kuanzisha au kuendeleza shughuli zao za
maendeleo.
0 comments:
Post a Comment