BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC KUJIULIZA KWA RUVU SHOOTING LIGI KUU YA VODACOM JAMHURI MOROGORO LEO.

Mlinzi wa Yanga Mbuyu Twite akimzuwia mshambuliaji wa Polisi Moro Nicolaus Kabipe wakati wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uwanja wa jamhuri Morogoro. 


TIMU ya soka ya Polisi Moro SC leo inashuka dimbani katika uwanja wake wa nyumbani wa Jamhuri kwa kucheza na Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara ambapo timu hizo zitahitadi ushindi ili kukwepa janga la kushuka daraja msimu huu.

Polisi Moro ambao Marchi 30 walitoa sare ya 0-0 na Yanga katika uwanja wa jamhuri ambapo mchezo wa leo wanahitaji kupata ushindi wa namna yoyote ili kuchumpa kutoka nafasi ya pili kutoka mkia na kusogea juu katika harakati za kujinasua na janga hilo.

Mwalimu wa Polisi Moro SC Mohamed Adolf Richard akizzungumza na JUMAMTANDA.BLOG alisema kuwa ushindi dhidi ya Ruvu Shooting utaifanya timu yake kuondoka katika nafasi ya pili kutoka mkiani na kusogea nafasi ya juu ili kukimbia mstari wa hatari ambao utawakumba timu tatu ambazo ndizo zitashuka daraja.

Richard alisema kuwa baada ya kutoa sare ya 0-0 na Yanga bado mahesabu yao yapo pale pale ya kuweka mikakati ya kukwepa kushuka daraja na nguvu wameelekeza katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kwa kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi wa namna yoyote ili kuweka sawa katika msimamo wa ligi hiyo ambayo inaenda ukingoni.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: