BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

STEVEN KANUMBA AKUMBUKWA.

Mwaka umepita tangu aliekuwa muigizaji nguli nchini, Steven Charles Kanumba afariki dunia kwa kifo cha ghafla. 
Kanumba atakumbukwa kama mmoja ya wasanii waliofanya tasnia ya filamu nchini izidi kukua na kupendwa hadi kuteka soko ambalo kwa kiasi kikubwa lilikuwa likishikiliwa na wasanii wa Nigeria. 
Aliondoka wakati bado hajayafaidi mafanikio na kushuhudia namna mapinduzi aliyofanya yalivyotengeneza ajira kwa vijana wengi, 
Pichani ni picha za kumbukumbu zake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
 Mama Kanumba akiweka shada lake la maua kwenye kaburi la mwanae
 Msanii Lulu akiweka shada la Maua katika kaburi la Steven Kanumba ambapo Lulu kwa sasa yupo nje kwa dhamana kufuatia tukio la kifo cha msanii huyo aliyefariki ghafla mwaka jana.
 Sehemu ya matukio ya Waigizaji  kwenye kumbukumbu ya Marehemu Kanumba makaburini Kinondoni
 Lulu na mama yake mzazi wakiwa katika makaburi ya Kinondoni
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: