BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

NJAMA ZA KUVURUGA KUAPISHWA KWA UHURU KENYATTA ZABAINIKA NCHINI KENYA.

Polisi wa kupambana na ghasia Kenya
Polisi wa kupambana na ghasia Kenya.Kenya's President-elect Uhuru Kenyatta attends a church service Mar. 31, 2013 at St Austin catholic church in Lavingtone, Nairobi.
 POLISI waonya dhidi ya njama zozote za kuvuruga sherehe za Jumanne za kumwapisha rais wa nne wa Kenya.
 
Polisi wa Kenya wamewataka  baadhi ya watu kuripoti kwa mkuu ya kitengo cha upelelezi (CID) Nicholas Kamwende kufuatia tuhuma kwamba wanapanga njama za kuvuruga sherehe za kumwapisha rais mteule, Uhuru Kenyatta kama rais wa nne wa Jamhuri ya Kenya siku ya Jumanne.

Inspekta Jenerali wa polisi David Kimaiyo amesema Jumapili kuwa kundi la vijana linapanga maandamano katika maeneo mbalimbali ya Nairobi ambayo hatimaye yatageuka kuwa ghasia wakati wa sherehe hizo za Jumanne.

Kimaiyo ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa polisi wana taarifa kwamba Jeckonia Junga Onyango, aliandaa mkutano na kukamilisha mpango wa njama hizo katika eneo la mabanda la Kibera nje kidogo ya Nairobi.

Taarifa za polisi huko Nairobi zinasema miongoni mwa maeneo yanayopangwa kufanyika maandamano hayo ni pamoja na Kibera, Kangemi, Kamukunji, Dandora na kariobangi.Vijana hao yaripotiwa wamepanga  kupora mali kuchoma mali na hata kushambulia wapinzani wao huku wakiwa na silaha kama vile mapanga. Bwana Kimaiyo ameonya kuwa uhalifu wa aina yoyote hutavumiliwa nchini humo.

Habari zaidi zasema waziri mkuu anayeondoka madarakani na ambaye alishindwa katika kinyang’anyiro cha urais katika uchaguzi uliopita. Raila Odinga amekwenda Afrika Kusini kwa mapumziko.

Taarifa kutoka kwa msemaji wake Dennis Onyango zinasema . 

Odinga hataweza kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Uhuru Kenyatta Jumanne licha ya mwaliko rasmi wa kuhudhuria sherehe hizo. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: