BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TEMESA YATENGEWA SH 20.8 MILIONI KWA AJILI YA MWAKA WA FEDHA WA 2013/2014.


Katibu mkuu wa wizara ya ujenzi, Balozi Mrango akifafanua jambo wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi la wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) inayowashirikisha wawakilishi wa wafanyakazi wa wakala kwa mikoa yote ya Tanzania bara inayoendelea katika ukumbi wa Glonency mkoani Morogoro.

WAKALA wa ufundi na umeme (TEMESA) imetengewa kiasi cha fedha Sh20.8milioni katika mwaka ujao wa fedha wa 2013/2014 na wizara ya ujenzi kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo kati ya fedha hizo zitaelekezwa katika shughuli mbalimbali.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wakala wa ufundi na umeme Mtendaji mkuu wa wakala wa ufundi na umeme (TEMESA) Mhandisi, Marcellin Magesa alisema kuwa serikali kupitia wizara ya ujenzi imeitengea taasisi ya wakala huyo kiasi cha Sh20.8milioni kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014 ambapo fedha hizo zitae

lekezwa katika upaji wa mishara na shughuli za kimaendeleo.

Magesa alisema kuwa kiasi cha sh20,879,199,258 milioni zinatarajia kupitishwa na baraza la wafanyakazi kwa ajili ya miradi ya kimaendeleo na shughuli mbalimbali.

Alifafanua kuwa kati ya fedha hizo kiasi cha sh15,682,730,000 milioni zitaelekezwa katika miradi ya kimaendeleo wakati mishara ni kiasi cha sh 4,965,240,000 milioni na sh 231,229,258 miliono matumizi ya kawaida ya kiofisi.

“Mkutano wetu wa baraza la wafanyakazi wa mwaka 2012/2013 lakini baraza hili linafanyika baada ya kukamilika kwa maandalizi ya mpango wa bajeti ya wakala kwa mwaka 2013/2014 pamoja na mambo mengine baraza hili litajadili na kupitisha bajeti ya wakala kwa mwaka wa fehda 2013/2014.” Alisema Magesa.

Naye Katibu mkuu wa wizara ya ujenzi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, Balozi Mrango alisema kuwa mkutano huo ni moja ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria yenye lengo la kuwashirikisha watumishi wa Temesa katika maamuzi yanayohusu maendeleo.

Mrango alisema kuwa mkutano huo utatoa fursa ya kujadili mambo ya msingi ya wakala na kutoa suluhisho la changamoto mbalimbali zinazoukabili wakala pamoja na kujadili bajeti ya wakala kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.

Mkutano huo unashirikisha wafanyakazi wa ufundi na umeme Temesa kutoka mikoa yote ya Tanzania bara unaofanyika mkoani Morogoro kwa siku mbili.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: