Afisa
nyuki wilaya ya Mvomero, Oscar Kunambi (katikati mwenye mavazi maalum)
akishirikiana na mkufunzi wa Joseph Mrindoko kulia wakitoa somo namna ya
kulina asali wakati wa mafunzo ya ufugaji nyuki yaliyofanyika katika
ukumbi wa shule ya sekondari ya Nassor Seif kwa kikundi cha Tumekubali
Women Group cha mji mdogo wa Madizini tarafa ya Turiani wilayani Mvomero
mkoani Morogoro.
Wanakikundi cha Tumekubali Women Group cha mji mdogo wa Madizini tarafa ya Turiani wilayani Mvomero wakiwa katika mafunzo ya ufugaji nyuki yaliyofanyika kwenye ukumbi wa sekondari ya Nassor Seif katika mji mdogo wa Madizini tarafa ya Turiani wilayani Mvomero mkoani Morogoro.
Na Juma Mtanda.
IMEBAINIKA kuwa ugonjwa wa uvimbe katika ubongo wa binadamu unaweza kutibiwa na kung’atwa na mdudu nyuki tiba ukiwemo na ugonjwa wa kichomi ikiwa njiamojawapo la kutatua uginjwa huo.
Akizungumza katika wakati wa mafunzo ya ufugaji nyuki Afisa Nyuki wilaya ya Mvomero mkoa wa Morogoro Oscar Kunambi alisema kuwa licha ya faida zinazopatika kwa nyuki mdudu huyo ana faida nyingi ikiwemo kutibu ugonj
wa wa ubongo wa binadamu na kichomi.
Kunambi alisema kuwa tiba ya ugonjwa wa ubongo wa binadamu ni lazima ung’atishwe katika kivundo cha mkono kuanzia nyuki mmoja hadi sita ndani ya wiki moja au mbili.
“Binadamu anatakiwa kung’atwa na nyuki mara moja kwa mwaka nah ii ni tiba kwa ugonjwa wa kichomi lakini pia nyuki huyo huyo huponyeshaa kabisa ugonjwa wa uvimbi wa ubongo wa binadamu ambapo dozi yake huchukua wiki moja ama mbili ili kumaliza tatizo hilo la uvimbe kichwani”. Alisema Kunambi.
Naye Katibu wa kikundi cha Temekubali Women Group cha mji mdogo wa Madizini tarafa ya Turiani wilayani Mvomero mkoa wa Morogoro, Zainabu Mbombe alisema kuwa mafunzo hayo yamewasaidia kufahamu faida nyingi zinazotokana na mdudu nyuki.
Mbombe alisema kuwa moja ya faida hizo ni namna ya kufuga nyuki na kupata mazao mbalimbali hivyo lengo la kikundi chao ni kutumia mafunzo hayo kuanzisha mradi wa ufugaji nyuki.
“Tayari kikundi chetu tumepokea fedha kutoka kwa Tanzania forest fund (TFF) kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ufugaji nyuki ambapo kwa sasa tupo katika awamu ya kwanza ya maandalizi ya kuandaa masanduku 60”. Alisema Mbombe.
Kikundi hicho kinatapokea fedha katika awamu tatu, awamu ya kwanza tayari imepokea fedha kwa ajili ya mafunzo wakati awamu ya pili itapokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabanda ili kuweka mizinga huku awamu tatu itapokea fedha kwa lengo la ununuzi wa mizinga 60 na ifika mwezi juni tayari mizinga itakuwa imeanza uzalishaji.
Mafunzo hayo ya siku mbili ambayo yameandaliwa na kikundi hicho cha Temekubali Women Group tayari wameanza kupokea mizinga mitano kutoka kwa waziri mkuu Mizengo Pinda ambapo kufikia mwezi juni kazi ya uzalishaji itakuwa imekamilika.
0 comments:
Post a Comment