BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WASIRA KATUMWA AU KAPAYUKA PALE BUNGENI DODOMA ?.

Uhuru hauna kikomo, Kikomo kinawekwa na maadui wa Uhuru. http://ndimara.blogspot.com

Kazi ya Usalama wa Taifa ni nini (TISS) ?.
WAZIRI wa mahusiano Ikulu, Steven Wassira amefanya kazi nzuri bila kujua.
Ni wakati alipouliza, mjini Dodoma, “Kibanda ni nani” hadi afanyiwe unyama kama aliofanyiwa.

1.  Kauli ya Wassira imeonyesha kuwa KWELI Idara ya Usalama wa Taifa "hushughulikia" watu fulani; jambo ambalo wamekuwa na kigugumizi kusema. Sasa amelitoa. 

Ambalo hakusema ni kushughulikia namna gani; lakini inaonyesha ni kama alivyofanyiwa Absalom Kiband, mhariri mkuu wa New Habari Corporation na mwenyekiti wa Jukwaa la Wahari – kupigwa, kung’olewa meno, kucha, kutobolewa jicho…

2. Wassira amesema Idara ya Usalama wa Taifa inaweza kushughulikia watu kama Dk. Slaa na Freeman Mbowe – viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema). 
Hakueleza kwanini; lakini tunajua ni kwa kuwa wanataka kushika madaraka – kuyatoa mikononi mwa CCM. 
Hili linazaa jambo lingine; kwamba
3. Sasa yeyote kati ya hao wawili atakayejikwaa, sharti tumtafute Wassira. Yawezekana hili lilimtoka kwa bahati mbaya au alikuwa na ghadhabu; lakini tayari tunalo. 
Kwamba hawa ndio lengo la idara ya usalama wa taifa na si mwingine, angalau kwa sasa. 

4. Lakini uwindaji haumo katika Chadema peke yao. 
Upo pia ndani ya CCM. Tuweke masikio tayari kusikia ni akina nani ndani ya CCM ambao wataelekezewa usalama wa taifa kwa kuwa hawako pamoja na mrengo mkuu. Chanzo chetu, bila shaka, kitakuwa Wassira.

5. Sasa Kibanda ni nani? Anauliza. Tusimpe jibu. Tuseme tu kwa sasa, kwamba, kama usalama wa taifa wana uwezo wa kushughulikia wakubwa, sembuse wadogo kama Kibanda.
Tumwachie Wassira kazi ya kumweka Kibanda pale anapoweza kumweka au aulize usalama wa taifa ambao wanaweza kumwambia mara moja.

6. Tusilokuwa na uhakika nalo ni kama Wassira alitumwa kuweka hadharani kwamba Slaa na Mbowe wanaandaliwa "kitu" na usalama wa taifa. Yawezekana amepayuka, jambo ambalo linaweza kumweka pabaya; au kaagizwa na hivyo atapewa nishani kwa “ujasiri” wa kutoboa siri.
7. Tusubiri. Tutaona.
ndimara
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: