http://www.habarimpya.com
KLABU ya Yanga imeanza kutakata katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, baada ya kuwa mbele kwa bao moja dhidi ya timu ya JKT Ruvu,
katika mechi inayoendelea kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Bao la Yanga limefungwa na Simon Msuva katika dakika 44 ya kipindi cha kwanza, baada ya kuwashindwa mabeki wa JKT Ruvu kabla ya kuachia shuti kali iliyomsindwa kipa Shaban Dihile.
Kabla ya bao hilo timu zote mbili zilikuwa zikicheza mpira wa kasi huku Yanga ikionekana kupwaya katika shemu ya kiungo na kuiruhusu JKT Ruvu kupenya kwa kasi lakini tatizo la umaliziaji ndiyo iliyowafanya washindwe kupata bao la kuongoza katika kipindi cha dakika 45 za kwanza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kutafuta ushindi lakini bahati ikawa kwa wanajangwani baada ya Hamis Kiiza kupachika bao la pili dakika 58.
Wakati maafande hao wakijiuliza kama wavue viatu vyao na kuvaa kandambili za mjini, wakapachikwa bakora ya tatu kutoka kwa Nizar Khalfan dakika 64 ndipo waliposalimu amri na kuamua kuvua buti na kuvaa malapa.
Mpaka mwamuzi wa mechi hiyo Oden Mbaga anapuliza kipenga cha mwisho Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 3-0, matokeo hayo imeifanya Yanga ifikishe pointi 56 na kubakiza pointi moja tu ili itawazwe kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
0 comments:
Post a Comment