Kwa ufupi
Wamesema licha ya Bunge kuongozwa na kanuni, wakati
mwingine viongozi hao wa Bunge wanatumia kanuni hizo kuwapendelea
wabunge wa CCM, huku wakieleza kuwa licha ya wabunge wa chama hicho
kutukana, hawakupewa adhabu yoyote. http://www.mwananchi.co.tzSpika wa Bunge Anna Makinda akiteta jambo na Naibu wake Job Ndugai.
BAADA ya Spika wa Bunge, Anne Makinda kutoa mwongozo na kuunga
mkono uamuzi wa Naibu wake, Job Ndugai kuwasimamisha wabunge sita wa
Chadema, wasomi, wanasiasa na wanaharakati wamesema Kiti cha Spika ndiyo
chanzo cha mvutano bungeni kwa kuwa kinapendelea wabunge wa chama
tawala (CCM).
Wamesema licha ya Bunge kuongozwa na kanuni,
wakati mwingine viongozi hao wa Bunge wanatumia kanuni hizo kuwapendelea
wabunge wa CCM, huku wakieleza kuwa licha ya wabunge wa chama hicho
kutukana, hawakupewa adhabu yoyote.
Jumatano ya wiki hii, Ndugai aliwasimamisha Tundu
Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Mchungaji
Peter Msigwa (Iringa Mjini), Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiah Wenje
(Nyamagana) na Godbless Lema wa Arusha Mjini kutohudhuria Bunge kwa siku
tano kutokana na alichokiita kufanya vurugu ndani ya Bunge.
Uamuzi huo wa Spika Makinda ulikuja baada ya
Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kumtaka
Ndugai aeleze alitumia kanuni gani kuwasimamisha wabunge hao.
Licha ya wabunge hao kupewa adhabu hiyo baada ya
kuomba mwongozo wa Spika na baada ya kupinga mwenzao kutolewa ndani ya
ukumbi wa Bunge, wapo wabunge wa CCM waliotukana na kutoa lugha za
kukera lakini hawakuchukuliwa hatua yoyote.
Wabunge hao ni Peter Serukamba ambaye alitukana
tusi zito la nguoni kwa lugha ya kimombo wakati ulipozuka mzozo wakati
wa hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Profesa Kulikoyela Kahigi.
Wengine ni mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia, Mwigulu Nchemba (Iramba Magharibi) na Livingstone Lusinde (Mtera).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na Mwananchi
Jumapili jana, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Profesa
Gaudence Mpangala alisema, “Bunge la sasa linakabiliwa na mambo mawili
makubwa; la kwanza ni udhaifu wa kiti cha Spika na pili ni wabunge wa
CCM kuamini kuwa Chadema ni maadui wakati katika hali ya kawaida siasa
ni ushindani na ndiyo demokrasia kwa kuwa sasa tuko katika mfumo wa
vyama vingi.”
Alisema kuwa Spika na Naibu wake wameshindwa kudhibiti vurugu bungeni kwa sababu ya kuendekeza itikadi za vyama.
“Kushindwa huko ndiyo kunachangia vurugu kwa
sababu wote wanaegemea upande mmoja, wabunge wengine wa upinzani
hawawezi kukubaliana na hali hiyo na huo ndiyo mwanzo wa malumbano,”
alisema Profesa Mpangala.
Alisema tatizo jingine ni kitendo cha wabunge wa
CCM na chama chao kudhani kuwa upinzani ni uadui, “Hayo ndiyo matunda ya
mfumo wa vyama vingi.
Mfumo huu ni wa ushindani na kuna mambo ya msingi yanayotolewa na wapinzani na mengine hayana ubaya wowote.”
Mfumo huu ni wa ushindani na kuna mambo ya msingi yanayotolewa na wapinzani na mengine hayana ubaya wowote.”
Mhadhiri mwingine wa Chuo hicho, Bashiru Ally
alisema Spika anaongoza Bunge kwa ushabiki wa vyama;
“Hatuwezi kutenganisha tabia za wabunge ndani na nje ya Bunge, ila pamoja na hilo bungeni sasa kuna ushabiki wa vyama.”
“Hatuwezi kutenganisha tabia za wabunge ndani na nje ya Bunge, ila pamoja na hilo bungeni sasa kuna ushabiki wa vyama.”
0 comments:
Post a Comment