WAZIRI wa sheria wa Misri, amejiuzulu kufuatia kilio
cha wafuasi wa kiisilamu kwa rais Mohammed Morsi kutaka idara ya sheria
kufanyiwa mageuzi makubwa.
Alitishia kuondoka serikalini mwaka jana baada ya rais kujilimbikizia mamlaka makubwa zaidi.
Maelfu ya wafuasi wa Morsi, waliandamana siku ya Ijumaa wakitaka wale waliokuwa katika utawala wa Mubarak kuondolewa katika nyadhifa za kisheria.
Maandamano yalikumbwa na ghasia wakati waandamanaji walipokabiliana na polisi
Mswaada tatanishi.
Katika barua yake ya kujiuzulu, bwana Mekky, alisema kuwa mikutano ya hadhara iliyofanywa mapema wiki hii ndiyo iliyochangia uamuzi wake.
Rais Morsi kwa sasa bado hajatamka lolote kuhusu tangazo hilo.
Aidha Rais Mohammed Morsi, amekabiliwa na matatizo chungu nzima, tangu kuingia mamlakani mwezi Juni mwaka 2012
Bwana Mekky, pia alielezea wasiwasi kuhusu juhudi zake kupitisha mswaada mpya ambao wakosoaji wanasena unaweza kupatia chama tawala cha muslim brotherhood udhubiti zaidi wa idara ya mahakama.
Mswaada huo unataka umri wa majaji kustaafu kupunguzwa , hatua ambayo itaamanisha kustaafishwa kwa lazima kwa majaji elfu tatu.
Hatua ya kujiuzulu kwa jaji huyo inakuja siku moja baada ya rais Morsi kutangaza mipango ya kufanyia mageuzi baraza la mawaziri.
Pamoja na mgogoro kutokoka katika idara ya mahakama, maandamano ya mageuzi yamekuwa yakifanyika kama vile yale ya kumpinga rais Morsi wakati wa kuadhimisha miaka miwili ya utawala wake tangu kung'olewa kwa Mubarak.
0 comments:
Post a Comment