Wapiganaji wa kundi wa Kiislamu la Boko Haramu.
ZAIDI ya raiya mia moja na themanini na tano
wamefariki huku nyumba elfu mbili zikiharibiwa kutokana na mapigano
makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Kiislamu kaskazini Mashariki mwa
Nigeria.
Jeshi na maafisa wa serikali wanasema kuwa kulikuwa na mashambulizi ya gurunedi, zilizosukumwa na roketi na makabiliano ya risasi katika mji tulivu wa Baga unaopakana na Chard Ijumaa jioni.
Wakazi walikimbili misituni na kurejea hapo jana ila walipata sehemu kubwa ya mji huo imeharibiwa na maiti na mizoga ikiwa imetapakaa kila mahali.
Mwanahabari mmoja amesema kuwa hali hiyo inadhirisha namna mapigano yamezidi Nigeria katika eneo la Kasikazini ambalo lina waislamu wengi.
Alisema wapiganaji walikuwa na silaha nzito kuliko zilizotumika katika mashambulizi ya hapo awali katika eneo hilo nao manusura wanasema washambuliaji wengi walikuwa wakizungumza lugha ya kigeni.
Inasemekana kuwa watu wengi zaidi wamefariki dunia ambapo bado juhudi za kutafuta maiti nyingine zinaendelea.
Brigedia Jenarali Austin Edokpaye amewaambia maafisa wakuu wa serikali kuwa,wapiganaji walitumia silaha kali na maroketi yenye mabomu mazito kupambana na vikosi vya jeshi.
Aidha bwana Edokpaye aliongeza kuwa,wapiganaji hao walikuwa wakitumia raia kama kinga yao kwa kujibanza karibu na makaazi ya watu ambapo walijua vikosi vya jeshi visingeweza kujibu mapigo.
Nigeria imekuwa ikikabiliwa na vifo vya raia wengi tangu kuibuka kwa vikundi vya wapiganaji wa kiislamu mwaka 2010 ambapo vingi vimejikita Kaskazini mwa nchi hiyo.
0 comments:
Post a Comment