Mlinzi wa Yanga Mbuyu Twite akimzuwia mshambuliaji wa Polisi Moro Nicolaus Kabipe wakati wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya 0-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara uwanja wa jamhuri Morogoro.
Picha JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA ya sh36.6Milioni zimepatikana katika mchezo wa Ligi kuu ya vodacom Tanzania baraa kati ya Polisi Moro SC na Yanga SC baada ya kuingiza watazamaji 7328 katika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Katibu mkuu mtendaji wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) Hamis Semka alisema kuwa jumla ya Sh36.640,000mil zimepatikana katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara baina ya wenyeji Polisi Moro SC na Yanga SC kutokana na watazamaji 7328 waliolipa kiingilio cha sh5,000 katika mchezo huo.
Semka alisema kuwa kati ya fedha hizo ziligawanywa katika makundi saba ambapo Polisi Moro SC na Yanga SC walipata mgao wa Sh8,207,472.45mil kwa kila timu huku Mamlaka ya mapato ikipata kiasi cha Sh5,589,152.54mil wakati ghalama za mchezo na mfuko wa maendeleo ya mpira (FDF) kila moja ikipata kiasi cha Sh2,503,976.17mil.
Alisema kuwa kiasi cha Sh4,173,293.62mil zimetolewa ikiwa ni ghalama za uwanja, wakati ghalama za tikiti ni Sh2,548,890mil, Kamati ya ligi ikipokea kiasi cha Sh2,503,976.17mil.
Katika mchezo huo uliokutanisha Polisi Moro SC na Yanga SC ulimazika kwa sare tasa ya 0-0 ambapo Yanga bado imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya vodacom kwa kukusanya pointi 49 huku Polisi Moro SC yenyewe ikiwa imekusanya pointi 18 na kushinda nafasi ya pili kutoka mkiani mwa msimamo wa ligi hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment