Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema akiwasili eneo la ajali mapema Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
Mwili wa
dereva wa lori moja kubwa lenye ujazo wa tani 18 ukiwa umeopolewa na
askari jeshi, tayari kupelekwa mochwari ya Hospitali ya Mt Meru. Dereva
huyu ametambulika kwa jina moja tu la Alex amefikwa na mauti akiwa ndani
ya gari hilo wakati vijana wengine wakiendelea kupakia moram asubuhi ya
leo
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo mbaya wakishangaa zoezi
la uokoaji na wengine wakisubiri kutambua ndugu zao, jambo ambalo
halikupata nafasi
Meya wa Manispaa ya Arusha, Mh Gaudence Lyimo akisaidiana na vikozi vya jeshi katika zoezi la uokozi
Mwananchi huyu aliishiwa nguvu baada ya kushuhudia mwili wa rafiki yake ukiopolewa kutoka kwenye kifusi
Hali ilivyo machimboni hapo
Kina mama wakilia kwa uchungu wakihofu kuondokewa na wapendwa wao
Sehemu ndogo ya Fuso ikionekana huku gari nyingine ikiwa haionekani kabisa
Ambulance ya Jiji tayari tayari kwa lolote ikihitajika
KWA
mujibu wa mashuhuda wa ajali iliyotokea leo asubuhi Jijini Arusha,
inakadiriwa zaidi ya watu 18 wamepoteza maisha kufuatia kufukiwa na gema
la mchanga/moram wakati wakichimba na kupakia kwenye malori.
Ajali
hiyo mbaya imetokea katika machimbo ya moram nje kidogo ya Jiji eneo
jirani na Moshono-Kiserian ambapo vijana hao wanaokadiriwa kufikia idadi
hiyo walikuwa wakipakia moram kwenye magari mawili, moja ni Fuso na
lingine kubwa zaidi (tani 18) na yote mawili yamefukiwa kabisa na
kifusi. endelea kupitia audifacejackson blogShuhuda
mmoja wa ajali ambae pia ni mchimbaji ameieleza Blog hii kwamba kwa
kawaida gari ndogo kama Fuso hupakiwa na watu 7, na hiyo kubwa huwa na
watu 12 bila kuhesabu dereva na utingo.
Blog hii
iliweza kushuhudia sehemu ndogo sana ya Fuso ikionekana lakini gari
nyingine ilikua imefukiwa kabisa na kupondeka vibaya. endelea kupitia audifacejackson blogMiongoni
wa waliofikwa na mauti ni pamoja na madereva wa magari hayo. taarifa za
eneo la tukio zinaeleza utingo mmoja ameokolewa akiwa amejeruhiwa
vibaya na kukimbizwa hospitali lakini dereva wake amefariki dunia.
Katika
eneo la ajali hali ni ya simanzi na vilio toka kwa kina mama huku baadhi
wa wababa na marafiki na ndugu wa jamaa waliofukiwa wakishindwa
kujizuia na kuangua kilio. endelea kupitia audifacejackson blog.
Meya wa
Manispaa Mh Gaudence Lyimo pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Godbless
Lema ni miongoni mwa viongozi wakubwa waliofika eneo la ajali kusaidiana
na kikosi cha Jeshi la Wananchi kufanya uokozi.
Blogu hii
ilishuhudia pia Wachina wakipeleka moja ya mashine zao (Excavator)
kuongeza nguvu katika kusaidia kufukua miili ya watu hao iliyonaswa na
kifusi hicho.
0 comments:
Post a Comment