Mshambuliaji wa Yanga SC, Didier Kavumbangu akiwatoka mabeki wa JKT Oljoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. |
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima (kushoto) akimtoka kiungo wa JKT Oljoro, mbele ya refa Amon Paul |
Didier Kavumbangu akigombea mpira na beki wa JKT Oljoro |
Hamisi Kiiza wa Yanga katikati akimtoka beki wa Oljoro kulia. Kushoto ni mshika kibendera namba moja, John Kanyenye akifuatilia mwenendo |
Frank Domayo kulia akipenyeza mpira pembeni ya kiungo wa Oljoro, Hamis Saleh |
Didier Kavumbangu akigombea mpira na beki wa Oljoro |
Didier Kavumbangu akiwania mpira wa juu dhidi ya beki wa JKT Oljoro nyuma yake. |
Didier Kavumbangu akiwa amemuangukia kipa wa JKT Oljoro, Mussa Lucheke huku beki Nurdin Mohamed akiondoka na mpira |
Sekeseke; Beki wa Oljoro akiwa hewani kupiga mpira wa kichwa wakati wa kizazaa langoni mwao |
Hamisi Kiiza akikosa bao baada ya kipa Mussa Lucheke kuokoa mpira ambao hata hivyo ulimponyoka... |
Hamisi Kiiza akijaribu kumpokonya mpira kipa wa Oljoro, Mussa Lucheke |
Kikosi cha Yanga. |
Kikosi cha JKT Oljoro. |
Simon Msuva akifumua shuti kufunga bao la pili la Yanga. |
Kiungo Athumani Iddi 'Chuji' akiwa ameruka na kipa wa JKT Oljoro, Mussa Lucheke. |
Wachezaji wa Yanga Nadir Cannavaro, Haruna Niyonzima na Athumani Iddi wakimlalamikia refa Amon Paul kushoto |
Said Bahanuzi wa Yanga akifumua shuti pembeni ya Hamisi Kiiza na beki wa JKT Oljoro, Salim Mbonde, Bahanuzi alifunga, lakini refa akasema alikuwa ameotea kabla ya kupiga mpira. |
0 comments:
Post a Comment