BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

YANGA YAITANDIKA OLJORO 3-0 NA KUIVUA RASMI UBINGWA SIMBA SC UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM



Pati la Ushindi; Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mfungaji wa bao lao la kwanza, Nadikr Haroub 'Cananavro' (katikati)

Na Mahmoud Zubeiry
YANGA SC imejitanua kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Kwa ushindi huo, Yanga imetimiza pointi 52 baada ya kucheza mechi 22, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 46, ambayo kesho itamenyana na Simba SC.  Aidha, Yanga pia kwa ushindi huo rasmi imeivua ubingwa Simba SC, ambayo haiwezi tena kufikisha pointi 52.


Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Amon Paul wa Mara, aliyesaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya na Anold Bugado wa Singida, hadi mapumziko, tayari Yanga walikuwa mbele kwa mabao 3-0.
Wauaji; Juu kulia Cannavaro (bao la kwanza), kushoto Msuva (bao la pili) na kulia chini Kiiza (bao la tatu) wakishangilia kwa staili tofauti mabao yao

Nadir Haroub ‘Cannavaro’ alikuwa wa kwanza kutikisa nyavu leo, akiunganisha mpira uliorudi kufuatia kona maridadi ya haruna Niyonzima dakika ya nne.


Simon Msuva alipokea pasi maridadi ya David Luhende akawapanguza mabeki wa JKT Oljoro kabla ya kufumua shuti kali umbali wa mita 19 na ushei lililotinga nyavuni dakika ya 16
Hamisi Kiiza alipokea pasi nzuri ya Niyonzima na kumlamba chenga kipa wa JKT kabla ya kuusukuma mpira nyavuni kuipatyia Yanga bao la tatu dakika ya 43.


Yanga ingeweza kutoka uwanjani baada ya dakika 45 za kwanza ikiwa ina mabao manne, iwapo bao la Niyonzima lisingekataliwa na refa Paul dakika ya 23.


Yanga ilipata pigo dakika ya 32 baada ya beki wa kulia Juma Abdul kuumia goti na nafasi yake kuchukuliwa na mkongwe, Nsajigwa Shadrack.


Kipindi cha pili, baada ya dakika mbili tu Oljoro ilipata pigo baada ya kipa wake Mussa Lucheke kuumia na kumpisha Shaibu Issa.
Uimara wa kipa mpya wa Oljoro uliizuia Yanga kupata mabao zaidi, licha ya kubadilisha karibu safu nzima ya ushambuliaji, Msuva akimpisha Nizar Khalfan na Kavumbangu akimpisha Said Bahanuzi.


Katika mchezo huo, kikosi cha Yanga kilikuwa; Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Nwsajigwa Shadrack dk 32, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva/Simon Msuva dk78, Frank Domayo, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbangu/Said Bahanuzi dk58 na Haruna Niyonzima.


JKT Oljoro; Mussa Lucheke/Shaibu Issa dk47, Yussuf  Machogoti, Majaliwa Sadik, Nurdin Mohamed, Shaibu Nayopa, Salim Mbonde, Karage Mgunda/Sixbert Mohamed dk67, Emmanuel Memba, Paul Nonga, Iddi Saleh na Hamisi Saleh.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: