RPC Mbeya Diwani Athuman
Na Esther Macha, Mbeya
WANAFUNZI
kumi na tano(15) katika shule ya sekondari ya Wazazi ya Lupata Wilayani
Rungwe Mkoani Mbeya wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuchoma
moto bweni la shule hiyo kutokana na wanafunzi wenzao kusimamishwa
masomo na uongozi wa shule kwa utovu wa nidhamu.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana ,Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani
Athuman alisema kuwa tukio lilitokea mei 14 mwaka huu majira ya saa 2.00
usiku katika shule ya sekondari Lupata.
Bw.Athuma
alisema kuwa wanafunzi hao baada ya kuona wanafunzi wenzao watatu
wamesimamishwa masomo walianza vurugu usiku na kuanza kuchoma moto
bweni moja la wanafunzi wa kiume .
Aidha
Kamanda Athuma aliwataja wanafunzi waliosimamishwa kwa utovu wa nidhamu
shuleni hapo kuwa ni ,Joseph Robert (18) Kidato cha nne Mkazi wa
Kitunda Jijini Dar es Salaam,Mwita Chacha(17),Mwanafunzi wa kidato cha
tatu mkazi wa Jijini Dar es Salaam ,pamoja na Daniel David(18)kidato
cha Tatu mkazi wa Ipinda Kyela.
“Hawa
wanafunzi watatu waliosimamishwa masomo walihamasisha wenzao kuunga
mkono kupinga adhabu hiyo kwa kufanya vurugu na kuchoma bweni hilo la
wanafunzi”alisema Kamanda Athuman.
Alisema
kuwa bweni lilochomwa moto walikuwa wanaishi wanafunzi ambao hawakuwa
tayari kuunga mkono uvunjifu huo wa amani shuleni hapo.
Aidha Bw.
Athuman alisema kuwa kufuatia vurugu hizo vinara wawili wa vurugu hizio
wanashikiliwa na jeshi kwa mahojiano zaidi ambao ni ,Joseph Robert ,
Mwita Chacha huku watuhumiwa kumi na tano wanashikiliwa na jeshi hilo.
Kuhusu
vitu ambavyo vimeharibiwa Kamanda huyo alisema thamani halisi ya
uharibifu uliotokea bado kujulikana na kwamba hakuna madhara yeyote ya
kibinadamu yaliyotokea .
Hata hivyo
Bw.Athuman ametoa wito kwa jamii hasa wanafunzi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake
watatue matatizo kwa njia ya meza ya mazungumzo katika mamlaka husika
ili kuepusha madhara na hasara zinazoweza kujitokeza ambazo mara nyingi
wahanga wanakuwa ni wanafunzi wenyewe.
0 comments:
Post a Comment