KIKOSI CHA YANGA.KIKOSI CHA SIMBA
Belinda Masangula, Dar es salaam.
BARA la Afrika Kesho litasimama kwa dakika 90 kushuhudia pambano kali la watani wa jadi, mechi ya Yanga na Simba ambayo itapigwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam itaonyeshwa dunia nzima kupitia Super Spor
t.
Mechi hiyo ndiyo mechi pekee katika Bara la Afrika inayodaiwa kuingiza mashabiki wengi wenye uwezo wa kujaza uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ambao una uwezo wa kubeba watazamaji elfu 60,000 waliokaa.
Mbali na Ujazo wa Uwanja huo pia ndiyo mechi pekee inayodaiwa kuwa na kila mbwembwe, vituko vya kila aina na baada ya mechi mashabiki wa timu hizo kongwe nchini Tanzania hutoka uwanjani na kushikana mikono kuelekea katika makazi yao bila vurugu za aina yoyote.
Wakati mashabiki na viongozi mbalimbali wa timu hizo wakiwa katika mazingira ya kushangilia ushindi, hali tete zaidi iko katika benchi la ufundi la Yanga ambalo wameshapokea taarifa kutoka kwa wazee wa klabu hiyo, pamoja na tajiri wao Yusuf Manji ya kwamba wasipo ibuka na ushindi katika mechi hiyo,hawatafanya sherehe za ubingwa.
Wakati hayo yakijiri, wadau mbalimbali wa soka nchini wametoa maoni yao juu ya mechi, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba Yanga itaibuka na ushindi mnono na wanaweza kulipiza idadi ya mabao matano waliofungwa mwaka jana.
"Simba si timu ya kutisha, wanacheza mpira wa kawaida kabisa tena wanatumia vijana ambao bado hawaa uzoefu wa kupambana na wachezaji wakongwe kama akina Haruna Niyozima, Athuman Iddi (Chuji), Nadir Haroub (Canavaro), na wengine wengi ndani ya Klabu hiyo"alisema Mkwasa katika mahojiano maalum na Habarimpya.com.
Mbali na kauli hiyo ya Mkwasa, baadhi ya mashabiki wa Yanga pia walitabiri ushindi mwepesi katika mechi hiyo lakini wakaitaka safu ya ushambuliaji kuwa makini na Beki wa Simba Shomari Kapombe, ambaye walidai kwamba anaweza kuizuia safu hiyo kutokana na umahiri wake wa kupambana na washambuliaji wazoefu.
Joshua Mussa ni shabiki wa Simba ambaye alidai kwamba safu ya Ulinzi ya Simba inapaswa kumchunga kiungo mshambuliaji wa Yanga Niyonzima, na wakifanikiwa hapo basi wataweza kupata ushindi katika dakika 45 za awali na baadaye kurudi Uwanjani katika dakika 45 za mwisho wakiwa na nguvu mpya.
http://www.habarimpya.com
0 comments:
Post a Comment