AMHENYESHA MTHAILAND VILIVYO. AUMIZWA MKONO KWENYE RAUNDI YA 6.
TANZANIA imetengeneza historia mpya
kwenye ngumi za kulipwa nchini Thailand baada ya mabondia wake kuwa
wanapigwa kila mara wanapokwenda kuiwakilisha nchi na bara la Afrika.
Safari hii JEMBE, kijana mtanashati anayeinukia kwenye masumbwi Jonas
Segu kutoka katika ukumbi wa mazoezi wa Respect Gym Boxing Club ya
Mabibo Loyola chini ya kocha Christopher Mzazi ameonyesha kipaji kikubwa
cha kusukuma msumbwi alipoushangaza umati wa maelfu ya wananchi wa
Thailand pamoja na nchi za ukanda wa Indo-China.
Segu alikuwa anachuana na bingwa wa IBF katika mara la Asia Pacific
Patomsuk Pathompothong kutoka Thailand katika uzito wa Light Welter
ambaye ni bondia namba 7 duniani katika viwango vya IBF.
Mpambano wao
ulifanyika katika jiji lenye mahekalu ya dhahabu la Bangkok na kurushwa
na television katika nchi zote za ukanda wa Indo-China za Laos, Myanmar,
Cambodia, Vietnam na Thailand yenyewe.
Mpambamo wa Segu na Pathompothong ulianza kwa bondia wa kitanzania
kuchomoka kama upinde kwenye kona yake na kumshambulia Pathompothong kwa
makonde mazito ya kumshikisha adabu. Segu alitupa makonde ya
mchanganyiko na kumzidi Pathompothong kutokana na uzito na umakini wa
ngumi zake.
Kwa kipindi chote cha raundi ya kwanza ilimbidi
Pathompothong ajilinde na kukimbia akizunguka ndani ya ulingo ili
kudhoofisha masumbwi ya Segu aliyekuwa anayachanganya kama mashine ya
kukomboa mpunga ambao unalimwa kwa wingi nchini Thailand!
Jonas Segu alikuwa chini ya uangalizi makini wa bondia maarufu mstaafu
George “Lister” Sabuni ambaye aliweza kumpa maelekezo ya nini cha
kufanya kwenye mpambano huo wa mwaka. Katika raundi ya 2, 3 na 4 Segu
aliuonyesha umati wa mashabiki wa Thailand kuwa yeye kweli ni bingwa
mtarajiwa na hakwenda Thailand kula wali wao ila kuiwakilisha nchi yake
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Segu alimhenyesha Pathompothong
vilivyo kwa kumchakaza kwa makondde mfululizo hususan akiutumia mkono
wake hatari wa kulia ambao ulionekana dhahiri kuwa unaleta madhara
makubwa kwa Pathompothong.
Ilididi timu ya wataalam wa Pathompothong kutafakari namna ya kumdhibiti
kijana huyo wa Kitanzania ambaye kweli alionekana kuwa alienda Thailand
kuuchukua mkanda wa IBF Pan Pacific na sio kufuata ulaji!
Raudi ta 5 Pathompothong aliingia ulingoni akiwa mtu tofauti kabisa
akirusha msumbwi mfululizo na kutembea ulingoni kama siafu huku akimvuta
Segu kenye kamba ili amkandamizie masumbwi yake.
Kijana huyo nadhifu wa
kitanzania (mwenye sura nzuri ya kuvutia na ambaye wasichana wengi wa
Thailand walishinda karibu na hoteli aliyoshukia ili kuweza kuongea
naye) alitumia wakati huo kumwonyesha Pathompothong kuwa yeye
hababaishwi na masumbwi yake kwani amefanya mazoezi ya kutosha.
Segu
alibadilishana masumbi na Pathompothong vilivyo na kuufanya umati wa
mashabiki waliojazana kwenye ukumbi huo kumshangilia kama vile yeye
ndiye bondia wao wakiimba Tanzania, Tanzania, Tanzania!
Katika raundi ya 6 mabondia wote waliingia ulingoni kama vifaru na
kubadilishana masumbwi ya mchanganyiko (combinations) wakitafuta
kudhibiti harakati za mpinzani mwenza.
Ni katika kubadilishana huku kwa
masumbwi ambako Segu aliumizwa mkono na Mthailand Pathompothong.
Inawezekana kuwa ni katika juhudi za kumzuia ili asiendelee kurusha
masubwi ya nguvu na kudhoofisha nguvu zake.
Kuumia mkono kwa Segu ilikuwa dhahiri kwani mwanzoni mwa raundi ya saba
wakati Pathompothong alipokuwa anamiliki ulingo dhidi ya kijana huyo
mtanashati wa kitanzania.
Katikati ya raundi ya saba Segu aliona kuwa
hawezi kuutumia mkono wake vizuri na kumwashiria refarii wa mpambano
kuwa anaacha !.
Segu aliacha pambano hilo katika raundi ya saba wakati mashabiki wengi
katika ukumbi huo wakiwa wanaimba Tanzania, Tanzania, Tanzania kwa jinsi
alivyokuwa anapeperusha vyema bendera ya “Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania”
0 comments:
Post a Comment