BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KILOMBERO YAVULIWA UBINGWA WA SOKA NA MANISPAA MASHINDANO YA UMISSETA MORO 2013

Mshambuliaji wa timu ya soka ya Manispaa ya Morogoro Jimmy Michael kulia akiwania mpiradhi dhidi ya mlinzi wa Morogoro Vijijini, Sconso James kushoto wakati wa mashindano ya shule za sekondari Tanzania (UMIS
SETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro yanayoendelea kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa, katika mchezo huo Manispaa ya Morogoro ilikubali kipigo cha bao 2-1. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
 Mshambuliaji wa timu ya soka ya Manispaa ya Morogoro Kassim Joseph kulia akimtoka mlinzi wa Morogoro Vijijini, Sconso James (kushoto chini)
Mlinzi wa timu ya soka ya Morogoro Vijijini Billalo kulia akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa timu ya soka ya Manispaa ya Morogoro, Richard Jovit.


Na Juma Mtanda, Morogoro.
MABINGWA watetezi timu ya soka ya wilaya ya Kilombero imepoteza mchezo wake wa nusu fainali na kuipa nafsi ya timu ya Morogoro Manispaa kutinga fainali kufuatia kupokea kipigo katika mashindano ya michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa kwenye mchezo mkali na wenye upinzani kwa kutwandikwa bao 2-1 mchezo uliofanyika uwanja wa jamhuri mkoani Morogoro. 

Kilombero ambayo ni mabingwa wa michuano hiyo kwa mwaka 2012 iliambulia kichapo hicho kutoka kwa Manispaa ambayo iliingia katika hatua ya nusu fainali kwa kupenya katika tundu la sindano kupitia mabao ya washambuliaji hatayri, Thafa Reli na Adam Solomon huku bao la Kilombero likipachikwa wavuni na mshambuliaji, Optatus Lupekenya na kufanya mchezo umalizike kwa Manispaa kuibuka na ushindi wa bao 2-1. 

Timu ya soka ya wasichana ya mkuu wa wilaya ya Mvomero, Anthony Mtaka ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kuingia fainali baada ya kuilaza Morogoro Vijijini na kukata tiketi ya kucheza fainali huku Kilosa nayo ikiingia kwenye hatua ya fainali kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa michezo ya soka kwa wasichana kufuatia kuibuka na ushindi wa bao 4-3 kwa njia ya changamoto ya mikwaju ya penalti dhidi ya Kilombero kufuatia kutoka sare tasa ya 0-0 dakika za kawaida kumalizika. 

Katika mchezo wa wavu wavulana timu ya Manispaa imetinga fainali baada ya kuilaza Mvomero seti 2-0 huku Kilombero iliingia hatua ya fainali kwa kuilaza Ulanga kwa seti 2-0. 

Manispaa katika michezo ya basketiboli na netiboli zimejiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa michezo hiyo ikiwa inaongoza kwa kila timu ikiwa imejikusanyia pointi sita ikiwa imesaliwa na mchezo mmoja mmoja na endapo itashinda michezo hiyo itatwaa ubingwa huo.

Wakati katika mchezo wa mikono timu za Kilombero na Manispaa zimetinga fainali kwa upande wa wasichana ambapo Manispaa ilipita hatua hiyo kwa kuilaza Ulanga bao 9-6 huku Kilombero ikiingia kwa kuifunga Morogoro Vijijini kwa bao 11-9. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: