KUPITIA season mpya ya Clouds Fm, ndani ya so so fresh na fetty, Mh
Halima Mdee jana amefunguka juu ya swali aliloulizwa kuhusu story zilizosambaa
kuwa anashiriki mapenzi ya jinsia moj
a.
Hii ndo kauli yake.
"Unajua huwezi kuzuia watu kusema, na mimi huwa sihangaiki na watu
wanasema nini, lakini ukitaka kumjua Halima unaweza ukamchunguza kirahisi sana,
kwa kumuangalia alipotoka, historia yake na mahusiano yake, ambayo
mengine ni wazi sana watu walikuwa wanayajua.
"Watu wanapenda ku speculate
pale ambapo wanaona kitu ambacho hawataki kuona, sasa hilo swala lilishaandikwa
sana, nadhani walioandika baadae wakaja kuomba radhi kwasababu waligundua
wameandika kitu kisicho sahihi, probably kutokana na sauti yangu you know,
probably kutokana na tembea yangu, kwasababu mimi nimekulia kwenye familia ya
wanaume watupu umeona eeh.
"Mimi nimekuwa ni mpambanaji tokea utotoni, kwasababu nimezungukwa
na jeshi la kibabe, thats who iam, lakini mtu anaetaka kumjua Halima na ana
uhuru tu, hata akitaka niwatajie list ya watu wangu i can do that.
"Lakini sidhani kama is their damn business, cause ma life is
personal, na wakitaka kuchunguza wachunguze kwa mpango wao na watapata taarifa,
kwa uhuru tu, na wanaweza wakatoa tangazo kwamba jamani watu waliowahi kuwa na
uhusiano na huyu if any wajitokeze.
"Watajitokeza kama wapo upande huo, watajitokeza kwasababu sasa hivi
si dunia huru bana."
0 comments:
Post a Comment