BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS ZANZIBAR DK.SHEIN AZINDUWA TAWI LA CHUO CHA KUMBUKUMBU MWALIMU NYERERE ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwasili katika viwanja vya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar, akiongozana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Dk. Salim Ahmed Salim. kwa ajili ya uzinduzi wa Chuo hicho kilioko nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Bububu. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiweka jiwe la Msingi la Jengo la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar, kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Dk. Salim Ahmed Salim na kushoto Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif hamad.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika sherere za uzindizi wa Chuo cha Kumbkumbu ya Mwalimu Nyerere Bububu Zanzibar.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. John Magotti, akitowa historia ya Chuo hicho kwa Rais wa Zanzibar katika sherere za ufunguzi wa Jengo la Chuo hicho huko Bububu Zanzibar.
Rais wa Zanzibar ma Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akimsikiliza Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. John.Mogotti akihutubia na kutowamaelezo ya ujenzi wa jengo hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. Salim Ahmed Salim akizungumza katika uzinduzi huowa Jengo la Chuo hicho uliofanywa na Rais wa Zanzibar Dk. Shein.
MWENYEKITI wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya MwalimNyerere Dk. Salim Ahmed Salim, akimkabidhi zawadi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, katikati Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad,  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mshauri wa Kitaaluma kutoka Chuo cha Ardhi Dk. Stanslaus Ntiyakunze, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Jengo la Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalim Nyerere kilichoko Bububu nje kidogo ya mji wa Zanzibar,kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho Dk. Salim Ahmed Salim na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Dk. John Magotti.baada ya kulizinduwa jengo hilo.
MKUU wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalim Nyerere Dk.John Magotti, akitowa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akitembelea jengo la Chuo, kushoto Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar MaalimSeif Sharif Hamad.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mkuu wa Chuo Dk. John Magotti na Mwenyekiti wa Bodi ya ChuoDk. SalimAhmed Salim, wakimsikiliza Mwalimu wa ICT Julias Maungo, akitowa maelezo kuhusiana na darasa la ICT katika Chuo hicho.

WANAFUNZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Tawi la Zanzibar wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akihutubia baada ya kulifunguwa Jengo hilo.
 WAGENI waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein , akihutubia baada ya kulifunguwa Jengo la Chuo cha Mwalim Nyerere Tawi la Zanzibar.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: