HABARILEO.
WAKAZI wa Mtwara wameaswa kuzungumza lugha moja ya amani, utulivu na
kujipanga vizuri ili nchi isije ikakosa fursa ya matunda yatokanayo na
gesi asilia.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesisitiza, kwamba yatakuwepo mabadiliko
makubwa si tu katika Mkoa wa Mtwara, bali mikoa mingine ya Nyanda za
Kusini kutok
ana na barabara, viwanda na huduma nyingine zitakazotokana
na uwepo wa malighafi hiyo.
Pinda ambaye amesema hakuna sababu ya kukamatana mashati, alisema
hayo jana wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha saruji
cha Dangote, mkoani humo.
Akielezea kampuni zilizojitokeza kuwekeza, Pinda alisema kutakuwa na
mitambo ya televisheni na redio ambayo kampuni tatu zimejitokeza
kutekeleza hilo.
Kampuni saba zimeamua kuwekeza katika usindikaji wa korosho, nyingine
zitawekeza katika maji ya kunywa. Kutakuwa na kiwanda cha mbolea
kinachowekeza katika bidhaa zinazotokana na mabaki ya gesi.
Kampuni nyingine itawekeza katika kiwanda cha kutengeneza mikate.
Aidha, kampuni mbili zitawekeza kwenye matangi ya kuhifadhi mafuta na
moja imeamua kujenga kiwanda cha ujenzi wa boti za uvuvi huku nyingine
ikiwekeza kwenye shughuli za mbao.
Bandari ya Mtwara inawezeshwa kuhudumia meli nne kubwa kwa wakati mmoja.
“Natamani na bandari ya Mikindani tuone namna ya kuiendeleza ibaki
kwa ajili ya abiria badala ya kubanana kwenye bandari kubwa,” alisema
Pinda.
Aidha, Waziri Mkuu alisema Serikali inazungumza na Serikali ya
Denmark na Korea Kusini kwa ajili ya kupata meli kubwa ya abiria na
mizigo itakayotoa huduma kati ya Mtwara na Dar es Salaam.
Vile vile itajengwa reli itakayosafirisha mizigo itakayoshushwa Mtwara kwa ajili ya mikoa ya Nyanda za Kusini.
Barabara.
Serikali imeendelea kuhakikishia wananchi kwamba barabara mbalimbali
ikiwamo ya Mtwara- Tunduru hadi Mbinga, wamewekwa makandarasi na ifikapo
mwaka 2017 iwe imekamilika.
Barabara ya Mangaka-Tunduru tayari zabuni zimeitishwa na wanahitajika
makandarasi wawili. Aidha, anatafutwa Mhandisi Mshauri kwa ajili ya
barabara ya Mtwara- Newala-Masasi itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Wakati wawekezaji zaidi ya 45 wameomba kuwekeza Mtwara kupitia Kituo
cha Uwekezaji (TIC), Waziri Mkuu alisema viwanda ambavyo viko tayari kwa
kujengwa mara moja ni cha mbolea aina ya Urea na cha dawa; ambavyo
vyote vitatumia malighafi ya gesi asilia ya Mtwara.
“Ili yote yawezekane, kinachohitajika ni amani. Bila amani haya yote
hayatawezekana,” alisema Pinda. Kiwanda kilichowekewa jiwe,
kitakapokamilika, kitazalisha mifuko 150,000 ya saruji kwa siku sawa na
tani milioni tatu kwa mwaka na kuajiri wafanyakazi 1,000.
Akizungumzia vurugu zilizotokana na upinzani dhidi ya kusafirisha
gesi kwa bomba kutoka Mtwara, Pinda alisema, “Hili kweli lilikuwa ni
jambo kubwa mpaka la kufika kukamatana mashati? Tangu tupate uhuru
tunachangiana”.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment