MWANANCHI, VIONJA VYA WIKI.
RASILIMALI ziwaunganishe, kuwaendeleza Watanzania wote na uvivu wa kudiriki ndiyo unaoitesa, kuiharibu sifa ya nchi yetu.
Hivi vilikuwa ni vichwa vya habari ambavyo niliviandika katika safu hii mapema mwaka huu nilipozungumzia suala linalofanana.
Suala hili ni gesi asilia iliyogundulika Mtwara na
Lindi na dhamira ya kuifikisha Dar es Salaam ambayo kwa sasa imegeuka
kiama, laana kwa nchi badala ya baraka zitokazo kwa Mungu.
Nilisema kuwa mijadala yote inayohusu mustakabali
wa nchi tangu kugundulika kwa rasilimali hiyo asilia umebadili
mwelekeo na kuiweka majaribuni Serikali ya Rais Jakaya Kikwete.
Nikaeleza pia kuwa wapo wanaiona rasilimali hiyo
kama baraka, njia ya nchi yetu kutokea, kuelekea kwenye neema na kuuaga
umaskini.
Ninakubaliana na maoni ya msomaji wangu aliyewahi
kuniandikia kwamba Tanzania kama jamii, lazima iweke msimamo au mfumo
wa pamoja wa jinsi ya kutu
mia vizuri rasilimali hizi ikiwamo gesi asilia, kwa kuzingatia umoja wake.
mia vizuri rasilimali hizi ikiwamo gesi asilia, kwa kuzingatia umoja wake.
Ni dhahiri wanasiasa, wanaharakati wote wanaozungumzia mradi huu kwa sasa hawana budi kuongozwa na mtazamo huu.
Hata hivyo, wasisahau kuwa walisoma au kusomeshwa
bure, kwa fedha za kahawa, pamba, mkonge na au almasi ya Mwadui kwani
hakukuwa na ubaguzi.
Inafaa wakumbuke kuwa wanaposhika bango kuhusu
gesi asilia kutosafirishwa kwa bomba kwenda miji kama Dar es Salaam na
mingineyo ambako ndiko kuna soko la uhakika, wasijisahau.
Hata wanaposhinikiza kwamba rasilimali hiyo ibakie
kusini wasisahau mgawo na mapato ya mazao yetu yaliyouzwa ndani na nje
kwa miaka mingi kupitia vyama vya ushirika, wakulima wakanufaika,
kiasi kilichobaki kikatengwa kwa shughuli za maendeleo katika maeneo
yote ya nchi, pia bila ubaguzi.
Ni kwa mfumo huo wa mazao ya biashara zama hizo,
bado naamini kuwa hata gesi asilia badala ya kung’ang’aniwa kuwa ibaki
kusini, inafaa iuzwe kokote Tanzania.
Gesi asilia iuzwe, viwanda vijengwe, mitambo ya
kufua umeme ijengwe pia Mtwara au Lindi kulingana na mahitaji, lakini
kiasi kinachotakiwa kufika Dar es Salaam kiachwe kiende.
0 comments:
Post a Comment