MTANZANIA.Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni
Akiuliza swali bungeni jana, Mbunge wa Viti Maalum, Magdalena Sakaya (CUF) alidai Katibu Mkuu huyo kwa kushirikiana na daktari katika hospitali hiyo walihamisha mashine hiyo na kuipeleka katika Hospitali binafsi ya Aga Khan.“
Lini Serikali itairudisha mashine ya kusafisha figo iliyohamishwa kutoka Muhimbili na aliyekuwa Katibu Mkuu kwa kushirikiana na daktari wa hospitali hiyo na kuipe
leka katika Hospitali ya ‘private?’, alihoji.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid alisema asingeweza kujibu swali hilo kwa kuwa hakuwa na taarifa kamili.
Naibu Waziri alisema kwa kuwa hana uhakika alimtaka mbunge huyo awalisishe upya swali lake litafutiwe majibu.
Awali akijibu swali la msingi la Sakaya, Dk. Rashid alisema hakukuwa na ongezeko la vifo vilivyohusishwa na moja kwa moja na mgomo wa madaktari wa Machi 2012 katika hospitali mbalimbali nchini.
Katika mgomo huo madaktari 394 waligoma na kati yao madaktari 376 walikuwa katika mafunzo kwa vitendo wakati madaktari 18 waliokuwa wameajiriwa walikutwa na hatia na kupewa onyo kali, alisema.
“Madaktari waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo waliondolewa katika vituo vya mafunzo na kutakiwa kuripoti kwa Baraza la Madaktari ambalo lilisimamisha usajili wao kuanzisha uchunguzi,” alisema.
Alisema baada ya uchunguzi madaktari waliofutiwa mashtaka kutokana na kukosekana kwa ushahidi ni 49, waliopewa onyo 213, onyo kali 66 na waliosimamisha kati ya mwezi mmoja hadi sita ni 30.
Walioahirishiwa mashtaka ni wanne na ambao hawakufika mbele ya baraza kujibu mashtaka ni madaktari 22, alisema.
0 comments:
Post a Comment