HABARILEO.
MCHUMI wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Elias Kitundu (39) amekufa
papo hapo huku mkewe Agness Msoka (37) na mtoto wao Samson Kitundu (17)
wakijeruhiwa, baada ya gari lao kugonga ‘treni ya Mwakyembe’ jana
alfajiri eneo la Moshi Baa Ilala, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo lililotokea saa 11.46 na
kuthibitishwa na Kamanda wa Kikosi cha Mamlaka ya Reli Tanzania na
Zambia (TAZARA), Rashid Seif, chanzo chake ni uzembe wa dereva wa gari
aliyekatisha reli wakati treni ikiwa karibu.
Ilielezwa kuwa lengo la dereva huyo ambaye ni mke wa marehemu,
alikuwa akiendesha kwa kasi gari hilo namba T 680 ARK aina ya Honda,
akiwahi kuvuka upande wa pi
li wa reli, ili kumwahisha mtoto wao
anayesoma Sekondari ya Airwing, ndipo ilipogonga treni na kusababisha
mauti ya mchumi huyo.
“Ilionekana dereva hakutaka ushauri wa mtu yeyote, kwani licha ya
watu kumpigia kelele na madereva wa magari mengine kumwashia taa
wakimtaka asimame, hakutaka kusikiliza ushauri huo,” alisema mmoja wa
mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Salum Makiya.
Mmoja wa wahudumu wa treni hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe
gazetini kwa kuwa yeye si msemaji, alisema akiwa ndani ya treni akitoa
huduma, alisikia kishindo na mkwaruzo na alipochungulia dirishani aliona
gari likikokotwa na treni umbali wa takribani meta 50 kabla ya
kusimama.
Kamanda Seif, aliitaja namba ya treni iliyohusika katika ajali hiyo
kuwa ni 5111 yenye injini namba BHF- 002, na ilikuwa ikiendeshwa na
David Ngonyani akisaidiwa na Moshi Hilary ikitoka Kipunguni kwenda Jet
Lumo.
Alisema ajali hiyo ilisababishwa na uzembe na kuthibitisha kifo cha
mchumi huyo kilichotokea papo hapo na mkewe na mtoto kujeruhiwa na baada
ya muda mfupi wote walikimbizwa katika Hospitali ya Amana.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana baadaye Amana, mtoto huyo
aliruhusiwa baada ya kupata matibabu ya michubuko huku mama yake
akihamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kutokana na majeraha aliyopata
yakiwamo ya kuvunjika miguu.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment