HABARILEO.Suzane Lyimo, ameunga mkono.
Hilda Ngoye.
Hilda Ngoye.
MJADALA mkali umeibuka miongoni mwa wabunge wakati wa kujadili Sera
ya Taifa ya Elimu na Mafunzo iliyowasilishwa na Serikali baada ya
kupinga tamko la kutaka umri wa kuanza elimu ya awali uwe miaka mitatu
huku wengine wakiunga mkono.
Wakati baadhi ya wabunge akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu, Suzane Lyimo
(Chadema) wakiunga mkono wakisema ni nzuri , wengine hususan Mbunge wa
Viti Maalumu, Hilda Ngoye (CCM) alipinga umri huo akisema ni md
ogo kwa
mtoto kuanza kufundishwa masomo ya darasani.
Ngoye aliungwa mkono na Mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine (CCM)
aliyesema sera hiyo imezingatia zaidi maeneo ya mijini kwani ni vigumu
kwa watoto wa vijijini wenye umri huo kutembea umbali mrefu kwenda
shule.
Aidha Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage (CCM) naye alisema
sera hiyo imejumuisha mazingira ya mijini na vijijini wakati ukweli ni
kwamba maeneo hayo ni tofauti.
Hoja hizo zilitolewa baada ya mtoa mada, Katibu Mtendaji wa
Shirikisho la Vyuo Vikuu nchini, Profesa Sifuni Mchome kueleza masuala
mbalimbali yaliyomo ndani ya sera hiyo. Mchome ndiye Mwenyekiti wa
Kamati iliyotunga sera hiyo.
Semina hiyo iliyohudhuriwa na viongozi wa juu wa Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, wakiongozwa na Waziri, Dk Shukuru Kawambwa na Naibu
wake, Philipo Mulugo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka pamoja na kusifu sera hiyo
lakini alisema lazima baadhi ya vipengele viangaliwe kwa kina kwa vile
umri wa mtoto kuanza shule ya awali akiwa na miaka mitatu na ule wa
miaka minne kwa mtoto kuanza shule ya msingi ni mdogo sana kwa kuanza
kumjaza mtoto masomo.
Wanaosifu Sera
Mbunge wa Viti Maalum, Suzan Lyimo (Chadema) alisema sera hiyo ni
nzuri akidai kuwa Serikali imeamua kuja na sera hiyo ambayo iliasisiwa
na Chama cha Demokrasia na Maendeleo.
Kwa mujibu wa Lyimo, walisisitiza elimu ya msingi na sekondari kuunganishwa kwa miaka 10 na kutolewa bure.
Kwa upande wake, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela
(CCM) alisema ameridhishwa kwa sera hiyo kuagiza watoto kuanza shule ya
awali na msingi wakiwa na umri mdogo kwa vile hatua hiyo itawezesha
watoto kuanza kujifunza katika umri mdogo na kuwa rahisi kwao kupokea
maarifa mapya.
Alisema hata hivyo ni lazima sera hiyo ikarejesha Mpango wa Kusoma,
Kuandika na Kuhesabu (KKK) kwa vile kuondolewa kwa Mpango huo ndiko
kulikofanya watoto sasa kumaliza darasa la saba na kuingia kidato cha
kwanza wakiwa hawajui kusoma na kuandika.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummi Mwalimu
alisema sera inapaswa kuboresha mazingira ya mtoto wa kike awapo shuleni
akisema hivi sasa watoto wa kike 8,000 wanakatisha masomo kila mwaka
kutokana na mimba huku watoto wengine wa kike wakikosa masomo kwa siku
saba kutokana na kufuata maji ya kutumia shuleni.
Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (CCM) pamoja na kukubaliana na
vipengele vya Sera hiyo, lakini alitaka Serikali kutilia mkazo suala la
utapiamlo.
Alisema tatizo hilo linasababisha wanafunzi kushindwa kujifunza huku
akisema hata kama sera hiyo itakuwa nzuri lakini kama suala la lishe
bora halitasisitizwa kwenye sera itakuwa ni kazi bure.
Profesa Mchome ajibu Akitoa majumuisho, Profesa Mchome alisema
ufahamu wa lugha kwa wanafunzi wa shule ya msingi, sekondari na vyuo
vikuu ni mdogo hivi sasa na kwamba ni wakati muafaka sasa kwa Serikali
kuwataka watoto kuanza shule wakiwa na umri mdogo ili waweze kuwa na
muda mrefu zaidi na mazingira bora ya kujifunza Kiswahili, Kingereza na
nyinginezo na kuboresha elimu.
0 comments:
Post a Comment