Mchezaji wa timu ya soka ya wasichana ya Ulanga, Finomena Mchungaredi (njano) akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Mvomero Fatuma Sahara wakati wa mashindano ya michezo ya shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro katika michezo ya ufunguzi yanayofanyika uwanja wa jamhuri mkoani hapa ambapo katika mch
ezo huo timu hizo zilitoshana nguvu ya bao 1-1.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mchezaji wa timu ya soka ya wasichana ya Ulanga, Frida Mtanga (njano) akiwania mpira dhidi ya mchezaji wa Mvomero Fatina Yusuph wakati wa mashindano ya michezo ya shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro
Na Juma Mtanda, Morogoro.
MASHINDANO ya michezo kwa shule za sekondari Tanzania (UMISSETA) ngazi ya mkoa wa Morogoro yameanza kutimua vumbi kwa michezo mbalimbali ya ufunguzi kwenye uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Katika michezo ya ufunguzi timu ya soka ya wavulana ya wilaya ya Kilombero ilianza vema michuano hiyo baada ya kuitandika Mvomero kwa ushindi wa bao 3-1 huku mchezo wa skoka wasichana Ulanga na Mvomero wakitoshana nguvu ya bao 1-1.
Kilombero ilipata bao yao kupitia kwa washambuliaji Optatus Yustine aliyepachika mabao mawili katika dakika ya 13 na 36 wakati bao la lingine likitumbukizwa wavuni dakika ya 21 na Jofrey Masima wakati bao la kufutia machozi la Mvemero likifungwa na Jordan Peter dakika ya 10.
Katika mchezo wa soka kwa upande wa wasichana Ulanga ndiyo walianza kupata bao katika dakika ya saba lililofungwa na Irene Masunda huku Mvomero wakisawazisha dakika ya 17 kupitia kwa Rehema Yuseph na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Michezo mingine kwa mchezo wa basketiboli wavulana Ulanga ilikubali kipigo cha vikapu 44-19 dhidi ya Kilombero wakati mchezo wa wavu Kilombero iliishinda Ulanga kwa seti 2-0 na Morogoro Vijijini waliibuka na ushindi wa seti 2-1 dhidi ya Ulanga.
Michezo hiyo inaendelea kufanyika kwenye uwanja huo wa jamhuri kwa michezo ya soka wavulana na wasichana, wavu wavulana na wasichana, basketiboli, netiboli, riadha, tufe, kurusha.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment